Thursday, March 9, 2023

MHE. RIDHIWANI KIKWETE AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WA IDARA YA UENDELEZAJI RASILIMALIWATU

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Idara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.

Watumishi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara ya Uendelezaji Rasimaliwatu (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Idara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Dkt. Edith Rwiza akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma. 

Afisa Utumishi Mkuu anayesimamia sehemu ya Mipango ya Rasilimaliwatu, Bi. Judith Shoo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya sehemu anayoisimamia kwa Naibu waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma. 


Afisa Tawala Mkuu anayesimamia sehemu ya Ushirikiano wa kimataifa, Bi. Mwanamridu Jumaa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya sehemu anayoisimamia kwa Naibu waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.


Afisa Tawala Mkuu anayesimamia sehemu ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bi. Marcella Mayala akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya sehemu anayoisimamia kwa Naibu waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.


No comments:

Post a Comment