Sunday, March 19, 2023

KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA YAMPONGEZA MHESHIMIWA RAIS KUWEZESHA UJENZI WA OFISI YA MAKAO MAKUU YA TAKUKURU DODOMA ITAKAYOIMARISHA MAPAMBANO DHIDHI YA RUSHWA

 

Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Tarehe 19 Machi, 2023

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kujenga ofisi Makao Makuu ya nchi Dodoma ambayo itaiwezesha taasisi hiyo kuimarisha mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa nchini.

Mhe. Dkt. Mhagama ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa ofisi ya makao makuu ya TAKUKURU jijini Dodoma, kwa lengo la kujiridhisha na utekelezaji wa bajeti iliyotegwa na Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23 ili kuiwezesha TAKUKURU kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Mhe. Dkt. Mhagama amesema, kwa ujumla kamati yake inampongeza sana Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ametoa kipaumbele cha kuziwezesha taasisi zote zinazotoa haki nchini ikiwemo TAKUKURU ambayo imepatiwa fedha kujenga jengo la makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dodoma.

Mhe. Dkt. Mhagama ameongeza kuwa, mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa ndio yataiwezesha nchi kufikia malengo ya maendeleo hivyo, mradi wa ujenzi wa ofisi ya TAKUKURU makao makuu ukikamilika kwa wakati utaiwezesha taasisi hiyo kutekeleza jukumu lake la msingi la kuzuia vitendo vya rushwa nchini.

“Sisi kama kamati tunatambua mchango na kazi kubwa anayoifanya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa akisadiwa na Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP Salum Hamduni,” Dkt. Mhagama amesisitiza.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema jengo hilo la ofisi ya makao makuu ya TAKUKURU jijini Dodoma linajengwa kwa kuzingatia majukumu yanayotekelezwa na TAKUKURU kwa mujibu wa Sheria.

Mhe. Jenista Mhagama ameongeza kuwa, katika jengo hilo, mifumo yote muhimu ya TEHAMA imewekwa kuiwezesha taasisi hiyo kufanya kazi kisasa na kukidhi viwango vya kimataifa vya taasisi zinazohusika na mapambano dhidi ya rushwa kama ilivyo kwenye mataifa mengine.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa ofisi ya TAKUKURU makao makuu Dodoma na kuhimiza mradi huo ukamilike kwa wakati ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo.

CP Hamduni amesema, kukamilika kwa ujenzi wa ofisi hiyo itakuwa ni chachu ya kuboresha na kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa nchini, ikizingatiwa kuwa hivi sasa watumishi wa TAKUKURU makao makuu wana changamoto ya ofisi kwani wanatumia majengo manne tofauti yaliyopo jijini Dodoma.

Serikali imetoa fedha kuiwezesha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007 ambayo ilianza kufanya kazi tarehe 01 Julai, 2007.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akizungumza mara baada ya kamati yake kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la TAKUKURU Makao Makuu jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifananua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la TAKUKURU Makao Makuu jijini Dodoma.

 


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakiwasili kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa jengo hilo Makao Makuu jijini Dodoma. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo pamoja na watendaji wa Serikali.

 

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo akichangia hoja kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa jengo hilo Makao Makuu jijini Dodoma.

 
 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiwa na wajumbe wa kamati yake wakimsikiliza Mshauri Mwelekezi kutoka Wakala ya Majengo Tanzania (TBA) alipokuwa akitoa maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa jengo hilo Makao Makuu jijini Dodoma. Wengine Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama na watendaji wa Serikali.

 

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria, Mhe. Tumaini Magessa akichangia hoja kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa jengo hilo Makao Makuu jijini Dodoma.

 

 

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria, Mhe. Khadija Taya akichangia hoja kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa jengo hilo Makao Makuu jijini Dodoma.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi, Salum Hamduni akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la taasisi yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa jengo hilo Makao Makuu jijini Dodoma.

Mwonekano wa mradi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Makao Makuu jijini Dodoma.

 

 

 

No comments:

Post a Comment