Friday, March 17, 2023

MHE. RIDHIWANI KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA IDARA YA TEHAMA SERIKALINI IKIWA NI MWENDELEZO WA VIKAO KAZI VYAKE VYA KUHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WA OFISI YAKE

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na watumishi wa Idara ya TEHAMA Serikalini (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Idara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.

Sehemu ya Watumishi wa Idara ya TEHAMA Serikalini wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma


Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma. 


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (meza kuu) akitazama mifumo ya TEHAMA inavyofanya kazi wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Idara ya TEHAMA Serikalini kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.


Afisa TEHAMA Mkuu, Bw. Faraja Komba akimpitisha Naibu waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kutazama mifumo mbalimbali ya TEHAMA ambayo imetengenezwa na Idara hiyo wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara ya TEHAMA Serikalini kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia Sehemu ya Viwango na Sera, Bw. Mohamed Mashaka akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya sehemu anayoisimamia kwa Naibu waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara ya TEHAMA Serikalini kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma. 



No comments:

Post a Comment