Na. Mwandishi wetu
“Fanyeni kazi kwa viwango vya juu hususani katika
ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma na majengo ya Serikali kwa kuzingatia
viwango vinavyostahiri ili tuweze kuaminiwa na kupata fedha za kuwekeza zaidi”
Maneno hayo yalisemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu kwa menejimenti ya Watumishi
Housing Investments (WHI) tarehe 19 Agosti, 2024 jijini Dar es salaam wakati alipofanya
ziara ya kujifunza namna taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake.
Mhe. Sangu alisema WHI inaamika katika kazi na sasa inapata zabuni za
kujega majengo na kusimamia kazi mbalimbali za ujenzi ikiwa kama mshauri mwelekezi,
hivyo wanastahiri pongezi.
Aidha, Mhe. Sangu ametumia kikao hicho kutoa maelekezo kwa menejimenti
ya WHI kuweka utaratibu mzuri wa kukusanya fedha kutoka kwa watumishi wa umma
waliokopeshwa nyumba ili fedha hizo ziweze kutumika katika ujenzi wa nyumba
nyingine za watumishi.
Aliongeza kwa kuwataka WHI kutengeneza utaratibu na kuingia Mikataba na Halmashauri
mbalimbali kwa ajili ya kupata maeneo na kujenga nyumba za bei nafuu kwa
watumishi wa umma.
Hali kadhalika, Mkurugenzi Mtendaji wa WHI Dkt. Fred Msemwa amesema
katika utekelezaji wa mpango wa makazi kwa watumishi wa umma zipo nyumba
zinazojengwa na kuuzwa na nyingine haziuzwi kwa kuwa Serikali inakuwa imetoa
fedha kwa ajili ya miradi maalum kwenye maeneo maalum na nyumba hizo hukabidhiwa
kwa walengwa.
Vile vile, amemshukuru Mhe. Sangu kwa kufanya ziara katika taasisi hiyo
na ameahidi yeye na menejimenti yake kutoa ushirikiano wa dhati wakati wote kwa
manufaa ya umma.
No comments:
Post a Comment