Wednesday, August 14, 2024

MAELEZO YA MUSWAADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA PCCB YAWASILISHWA KWENYE KAMATI YA BUNGE

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent L. Kyombo akizungumza na Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watendaji wa PCCB (hawapo pichani), wakati wa Kikao cha kamati hiyo cha kupokea maelezo ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa jijini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Viongozi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia wasilisho la maelezo ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akitoa neno la shukrani kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati baada ya wasilisho la maelezo y Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma.

Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa CP. Salum Hamduni wakifuatila wasilisho la Maelezo ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akiwasilisha Maelezo ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria (hawapo pichani) katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma.


Baadhi ya Viongozi na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakifuatilia wasilisho la maelezo ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma.

 



 








No comments:

Post a Comment