Thursday, August 22, 2024

NAIBU WAZIRI SANGU AWAASA WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA AJIRA KUWAJIBIKA

 Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 22 Agosti, 2024 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amewaasa Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuwajibika kwa viwango vikubwa katika kutekeleza majukumu yao ili kutimiza azma ya taasisi hiyo katika kutoa ajira kwa kutenda haki sawa kwa kila mwananchi.

Mhe. Sangu ameyasema hayo leo tarehe 22 Agosti, 2024 wakati alifanya ziara yake ya kikazi iliyolenga kujifunza majukumu ya ofisi hiyo na kuhimiza uwajibikaji.

“Niwaase kuwajibika kwa viwango vikubwa katika kutekeleza majukumu yenu hasa kwa kutenda haki sawa kwa kila mwananchi atakayeomba ajira, zingatieni maadili ya taasisi hii kwa maslahi ya taifa, amesema Mhe. Sangu”.

Aidha, Mhe. Sangu ameipongeza Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuboresha na kurahisisha usaili kwa kutumia TEHAMA kwani haki inatendeka na inaijengea taasisi uaminifu mkubwa kutoka kwa wananchi.

Mhe. Sangu ameendelea na ratiba yake ya kutembelea taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kujifunza kuhusu majukumu ya taasisi hizo na kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (wa kwanza kushoto) akizungumza na Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi.

Baadhi ya Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (meza kuu kulia) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi.


Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu alipokuwa akizungumza nao wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo.


Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, ambaye ni Mkuu wa Idara ya TEHAMA, Mhandisi Samwel Tanguye  (aliyesimama meza kuu) akielezea utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (aliyekaa kulia meza kuu) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akipokea maua ya ukaribisho mara baada ya kuwasili katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira zilizopo jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa ofisi ya Sekretarieti ya Ajira baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika ofisi hiyo iliyopo jijini Dodoma.











No comments:

Post a Comment