“Mfumo wa Kupima Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (e-Utendaji kazi) ni matokeo ya maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na ni utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma, hivyo ni lazima kila mtumishi wa umma kujiunga na kutumia mfumo huo na si hiari” amesisitiza Mhe. Sangu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu
ameyasema hayo leo tarehe 15 Agosti, 2024 wakati alipokuwa akifuatilia
mawasilisho mbalimbali ya majukumu ya Idara ya Usimamizi wa Mikataba ya
Utendaji Kazi Serikalini, Idara ya Usimamizi wa Maadili, Idara ya Usimamizi wa
Huduma za TEHAMA Serikalini na Idara ya Mipango ikiwa ni sehemu ya kujifunza
kuhusu majukumu ya Ofisi yake.
Mhe. Sangu ameelekeza Idara ya Usimamizi wa Utendaji Kazi Serikalini kufuatilia
watumishi wote wa umma mahali popote walipo ili kujua wanafanya nini na kwa
maslahi ya nani.
Aidha, ametoa rai kwa idara hiyo kufanya utafiti na kubaini taasisi ambazo zinasuasua
kutumia mfumo huo ili hatua za kinidhamu
ziweze kuchukuliwa dhidi ya Maafisa Maasuli na watumishi wa Taasisi hizo.
Kwa wakati mwingine ameelekeza Idara ya Usimamizi wa Maadili kutoa
mafunzo ya maadili kwa watumishi wapya na walio kazini ili waweze kutambua na
kujikumbusha misingi ya maadili katika utumishi wa umma.
“Kuna mambo yasiyofaa ambayo yako kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma
na yanaendelea katika ofisi za umma kutokana na watumishi hao kujisahau na
kuzifanya ofisi hizo kuwa binafsi.
Hali kadhalika, ameipongeza Idara ya Huduma za TEHAMA Selikani kwa
kubuni, kusanifu na kutengeneza mifumo ambayo inasimamia utendaji kazi katika utumishi
wa umma.
Mhe. Sangu ameendelea na ratiba yake ya kujifunza kuhusu majukumu ya
idara mbalimbali zilizopo katika ofisi yake yanayofanyika katika ukumbi mdogo
wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mtumba Jijini
Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akiptia
nyaraka wakati wa kikao cha kumpitisha katika majukumu ya Idara mbalimbali kilichofanyika
katika ukumbi mdogo wa Ofisi hiyo tarehe 15 Agosti, 2024.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akizungumza
na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini wakati
wa kikao cha kumpitisha katika majukumu ya Idara hiyo kilichofanyika katika
ukumbi mdogo ulipo jengo la Utumishi Jijini Dodoma leo tarehe 15 Agosti, 2024.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akimsikiliza
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Bw. Cosmas Ngangaji wakati wa kikao cha
kumpitisha katika majukumu ya Idara hiyo kilichofanyika Mtumba Jijini Dodoma
leo tarehe 15 Agosti, 2024.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akimshukuru
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Bw. Cosmas Ngangaji baada ya kikao cha kumpitisha katika majukumu
ya Idara hiyo kilichofanyika Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 15 Agosti, 2024.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akimsikiliza
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili Bi. Leila Mavika wakati wa kikao
cha kumpitisha katika majukumu ya Idara hiyo kilichofanyika Mtumba Jijini
Dodoma leo tarehe 15 Agosti, 2024.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akizungumza
na Idara ya Usimamizi wa Huduma za TEHAMA Serikalini wakati wa kikao cha
kumpitisha katika majukumu ya Idara hiyo kilichofanyika Mtumba Jijini Dodoma
leo tarehe 15 Agosti, 2024
No comments:
Post a Comment