Monday, August 5, 2024

WATUMISHI WA OFISI YA RAIS-UTUMISHI WAPIMA AFYA KWA HIARI

Watumishi wa Umma wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wameitikia wito wa kushiriki zoezi muhimu la upimaji wa afya wa hiari katika kambi ya uchunguzi, upimaji, tiba na ushauri wa afya zinazotolewa kwa watumishi wote wa Wizara na Taasisi za Umma.

Kambi hiyo inayoendeshwa na Wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa inafanyika katika Jengo dogo la zamani la Ofisi ya Rais-UTUMISHI lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Baadhi ya huduma zinazotolewa katika kambi hiyo ni pamoja na Saratani, Tiba Ukunga na Magonjwa ya akina Mama, Magonjwa ya Figo, Moyo, Macho, Masikio, Pua, Koo, Mifupa na Ajali

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeshirikiana na Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa katika kuratibu zoezi hilo ikilenga kuwafikia watumishi wa umma ili waweze kufahamu hali zao za afya na kupata ushauri wa kitaalam kutoka kwa Madaktari Bingwa.

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Leila Mavika akizungumza jambo na mtoa huduma kutoka Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa wakati alipowasili kushiriki zoezi la upimaji wa afya wa hiari katika kambi ya uchunguzi, upimaji, tiba na ushauri wa afya zinazotolewa kwa watumishi wote wa Wizara na Taasisi za Umma Mtumba jijini Dodoma.

Baadhi ya Waratibu wa zoezi la upimaji wa afya wa hiari kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa tayari kuwapokea watumishi wa umma kupima afya kwa hiari katika kambi ya uchunguzi, upimaji, tiba na ushauri wa afya zinazotolewa Mtumba jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bibi Hilda Kabissa akifurahia jambo na Daktari kutoka Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa wakati aliposhiriki zoezi la upimaji wa afya wa hiari katika kambi ya uchunguzi, upimaji, tiba na ushauri wa afya zinazotolewa kwa watumishi wote wa Wizara na Taasisi za Umma Mtumba jijini Dodoma.

Bi. Neema Range (kulia) na Bi. Sara Simule (kushoto) kutoka ofisi ya Rais-UTUMISHI wakipima urefu wakati wa zoezi la upimaji wa afya wa hiari katika kambi ya uchunguzi, upimaji, tiba na ushauri wa afya zinazotolewa na Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa kwa watumishi wote wa Wizara na Taasisi za Umma Mtumba jijini Dodoma.

Bi. Zaituni Magige kutoka ofisi ya Rais-UTUMISHI akipewa huduma ya kupima afya wakati wa zoezi la upimaji wa afya wa hiari katika kambi ya uchunguzi, upimaji, tiba na ushauri wa afya zinazotolewa na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa kwa watumishi wote wa Wizara na Taasisi za Umma Mtumba jijini Dodoma.

Watumishi kutoka ofisi ya Rais-UTUMISHI wakipatiwa huduma ya awali wakati wa zoezi la upimaji wa afya wa hiari katika kambi ya uchunguzi, upimaji, tiba na ushauri wa afya zinazotolewa na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa kwa watumishi wote wa Wizara na Taasisi za Umma Mtumba jijini Dodoma.



 








No comments:

Post a Comment