Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 10 Agosti, 2024
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka amezielekeza Ofisi za Umma kuwa na programu maalum ya michezo kwa Watumishi wa Umma ili kuimarisha afya zao na kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa ustawi wa taifa.
Balozi Dkt. Kusiluka amezungumza hayo leo tarehe 10
Agosti, 2024 katika Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika katika Uwanja wa
Jamhuri jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya michezo ya SHIMIWI inayotarajia
kuanza tarehe 18 Septemba hadi 05 Oktoba, 2024 mkoani Morogoro.
Balozi Dkt. Kusiluka ametoa rai kwa Wizara na taasisi zote za umma kutenga
bajeti na muda kwa ajili ya michezo kwa watumishi wa umma ili waweze kushiriki
kwa lengo la kuimarisha afya zao, kudumisha umoja na ushirikiano.
Aidha, Dkt. Kusiluka amempongeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw.
Juma Mkomi na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Gerson Msigwa
kwa kushiriki katika maandalizi ya bonanza hilo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu-UTUMISHI,
Bw. Juma Mkomi amesema kuwa agizo la Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka la kutaka Ofisi za
Umma kuwa na programu maalum ya michezo kwa watumishi wa umma ni jambo jema kwani
itawahamasisha zaidi kutunza afya zao na kuwawezesha kutekeleza majukumu na kutoa
huduma bora kwa wananchi.
Vilevile, Bw. Mkomi ameongeza kuwa
ofisi yake imekuwa ikishiriki kliniki za afya kwa watumishi wa umma ambapo hivi
karibuni ilishirikiana na Hospitali ya Benjamin Mkapa katika kambi maalum ya
zoezi la upimaji afya wa hiari katika maeneo ya ofisi za Serikali Mtumba lengo
likiwa kuimarisha afya za watumishi wa umma.
Viongozi na Watumishi wa
Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wameshiriki katika bonanza hilo ambalo hufanyika kila
mwaka, na Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Michezo
Huboresha Utendaji kazi, Shiriki Uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa
Taifa Endelevu.”
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Dkt. Moses Kusiluka (aliyesimama) akizungumza na Watumishi wa Umma walioshiriki katika Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri
jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akitoa salamu za ofisi yake wakati wa Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Dkt. Moses Kusiluka (wa kwanza
kushoto) akifanya mazoezi ya viungo wakati wa Bonanza la Michezo
ya SHIMIWI
lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi. Wengine ni Viongozi wa Serikali waliohudhuria
bonanza hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya
Mishahara, Posho na Marupurupu, Bi. Mariam Mwanilwa (wa kwanza kushoto) pamoja
na watumishi wa ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifanya mazoezi ya viungo wakati
wa Bonanza
la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika
Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Katibu Mkuu-UTUMSHI, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akizungumza
jambo na Katibu
Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Majula Mahendeka (kulia) wakati wa
Bonanza la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Bonanza la
Michezo ya SHIMIWI lililofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri
jijini Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI wakifanya mazoezi ya viungo wakati wa Bonanza
la Michezo ya SHIMIWI lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini
Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (aliyevaa traki nyeusi) akifurahia jambo na Wakurugenzi na
Watumishi wa ofisi yake mara baada ya kuhitimisha Bonanza la Michezo
ya SHIMIWI lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini
Dodoma.
No comments:
Post a Comment