Wednesday, August 28, 2024

SERIKALI INAFANYA KAZI KUPITIA NYARAKA - Mhe. Sangu

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amesema kuwa msingi mkuu wa ufanyaji kazi wa Serikali ni kwa kupitia nyaraka ambazo zinaisaidia Serikali kutimiza uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yake kupitia miongozo ya nyaraka hizo.  

Naibu Waziri Sangu, ameyazungumza hayo leo wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa iliyolenga kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri Sangu amesema kuwa utunzaji wa nyaraka kupitia Idara hiyo ni jukumu adhimu linalohitaji viwango vikubwa vya usimamizi ili kuleta haki na uwazi katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya Serikali kwa kutumia nyaraka hizo.

Aidha Mhe. Sangu ameipongeza Idara hiyo kwa namna wanavyofanya kazi kubwa ya kuwaenzi waasisi wa Taifa la Tanzania kwa kukusanya na kutunza kumbukumbu zao zitakazosaidia vizazi vijavyo kufahamu historia ya nchi kupitia waasisi hao.

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa vibali vya ajira na kuwezesha idadi ya watumishi kuongezeka kila mwaka kwa lengo la kuongeza ufanisi.

Naye, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bi. Editha Beda, wakati akitoa neno la shukrani amesema menejimenti imepokea maelekezo yote na kuahidi kuyafanyia kazi kwa ukamilifu ili kuongeza ufanisi katika utendajikazi kwa ustawi wa taifa.

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na viongozi na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji jijini Dodoma.

Baadhi ya watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofsi hiyo jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi akielezea utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji.

Baadhi ya watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofsi hiyo jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi (kulia) akimuonesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu moja ya nyaraka zinazohifadhiwa katika ofisi hiyo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji.


Afisa Kumbukumbu, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bi. Maryam Ayoub (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo.


Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo alipofanya ziara ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (aliyevaa tai nyekundu) akipata maelezo kuhusu namna ya kudurufu nyaraka mbalimbali kidijitali wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi hiyo.


Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bi. Editha Beda akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu mara baada ya kuhitimisha ziara ya kikazi katika ofisi hiyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (aliyevaa tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watendaji wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi.



No comments:

Post a Comment