Wednesday, August 28, 2024

VIONGOZI WASHIRIKI UFUNGUZI WA KIKAO CHA WENYEVITI WA BODI AICC

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simabachawene (Wa kwanza kushoto, mstari wa Pili) na viongozi wengine wakifuatilia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa kufungua Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma kinachofanyika katika ukumbi wa AICC, Jijini Arusha tarehe 28 Agosti, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali baada ya kufungua Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma kinachofanyika katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha tarehe 28 Agosti, 2024


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi akiwa katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma Kinachofanyika katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Kikao hicho kimefunguliwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 28 Agosti, 2024.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simabachawene akiteta jambo na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo  Mhe. Damas Ndumbaro wakati wakisubiri ufunguzi rasmi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma uliofaywa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha tarehe 28 Agosti, 2024.











No comments:

Post a Comment