Thursday, August 22, 2024

MHE. SANGU: SHUGHULIKIENI CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA UMMA

 Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 22 Agosti, 2024

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameitaka Tume ya Utumishi wa Umma kupokea na kushughulikia changamoto za watumishi wa umma kwa wakati ili kujenga imani kwa watumishi kupitia taasisi hiyo na kupata suluhisho la changamoto hizo kwa muda sahihi.

Naibu Waziri Sangu, ameyazungumza hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi ambapo amewatala kuwa wazalendo katika kutekeleza majukumu yao.

Aidha Mhe. Sangu ameitaka menejimenti hiyo kuongeza mawanda na kuwa na ubunifu katika kutoa huduma kwa watumishi ili kutoa uhuru wa kujieleza pale ambapo watumishi watahitaji kuwasiilisha changamoto au malalamiko mbalimbali.

Awali akitoa neno la utangulizi, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama amesema kuwa waajiri katika mamlaka za ajira na mamlaka za nidhamu wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Taratibu, Kanuni na Miongozo.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Idara ya Rufaa na Malalamiko, Bw. John Mbisso akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri Sangu amesema kuwa, menejimenti imepokea maelekezo yote na kuahidi kuyafanyia kazi kwa ukamilifu.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi hiyo jijini Dodoma.


Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji.


Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama akitoa maelezo ya awali kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu kabla ya Naibu Waziri huyo kuzungumza na Watendaji wa Ofisi hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi jijini Dodoma iliyolenga kuhimiza uwajibikaji.

Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Katibu Idara ya Rufaa na Malalamiko, Bw. John Mbisso akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu mara baada ya Naibu Waziri huyo kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika ofisi hiyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (katikati aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi jijini Dodoma iliyolenga kuhimiza uwajibikaji.  


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (wa kwanza kulia) akielekea kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma wakati wa ziara yake ya kikazi jijini Dodoma. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (aliyenyanyua mikono) akitoa maelekezo kwa mshauri elekezi wa ujenzi wa jengo hilo TBA mara baada ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma wakati wa ziara yake ya kikazi jijini Dodoma. 

Mwonekano wa jengo jipya la Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma ambalo ujenzi wake unaendelea jijini Dodoma









No comments:

Post a Comment