Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 07 Agosti, 2024
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya afya
ikiwemo Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa ili kuhakikisha watumishi wa umma
wanapata fursa ya kutambua hali zao za kiafya na kuchukua hatua stahiki kwa
lengo la kuongeza ufanisi kiutendaji.
Hayo yamesemwa leo na
Mwakilishi wa Katibu Mkuu - UTUMISHI ambaye
ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bw. Cyrus Kapinga wakati akizindua kambi maalum
ya uchunguzi wa Magonjwa Yasiyoambukizwa kwa watumishi wa umma uliofanyika katika
jengo dogo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mtumba jijini Dodoma.
Bw. Kapinga amesema Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala bora ambayo ndio msimamizi wa Utumishi wa Umma na
Utawala Bora ina wajibu wa kuhakikisha Taasisi za Umma zinatekeleza dhana ya
Utawala Bora ikiwemo kusimamia vema eneo la Menejimenti ya ujumuishwaji wa
Anuai za Jamii ikiwemo udhibiti wa VVU, UKIMWI na MSY mahali pa kazi katika
Utumishi wa Umma.
Aidha, Bw. Kapinga amewashukuru Viongozi wa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Wataalam wa afya kwa kushirikiana kuandaa kambi hiyo ambayo ni
muhimu kwa watumishi wa umma kwani asilimia kubwa huathirika na magonjwa
yasiyoambukiza pasipo wao kujua.
Pia amewapongeza waajiri wa Wizara na Taasisi zote
ambao wameridhia watumishi wao kushiriki zoezi hilo muhimu kwani mwitikio umekuwa
ni mkubwa.
Awali akitoa neno la utangulizi, Mkurugenzi Mtendaji
wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Profesa Abel Makubi ameishukuru Ofisi ya
Rais-UTUMISHI kwa kuratibu na kusimamia kwa kushirikiana na Hospitali ya
Benjamin Mkapa katika zoezi la Kambi ya Uchunguzi,
Ushauri na Elimu ya Afya kwa watumishi wa Umma katika Wizara, Taasisi na
sekta binafsi.
Naye, Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu,
Bw. Musa Magufuli amewashukuru Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa
kukubali kushiriki zoezi hilo la Kambi ya Uchunguzi, Ushauri na Elimu ya Afya
kwa watumishi wa Umma kwani mwitikio umekuwa mkubwa wa watumishi hao kutaka
kujua hali zao za afya.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora imeshirikiana na Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa katika
kuratibu zoezi hilo ikilenga kuwafikia watumishi wa umma ili waweze kufahamu
hali zao za afya na kupata ushauri wa kitaalam kutoka kwa Madaktari Bingwa.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ambaye
ni Mkurugenzi
wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bw. Cyrus Kapinga akizungumza
na Viongozi na Watumishi wa Umma wakati wa
uzinduzi wa Kambi ya Uchunguzi, Ushauri na Elimu ya Afya
uliofanyika katika jengo dogo la Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mji wa Serikali Mtumba
jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi Wasaidizi wa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na watumishi wengine wa Wizara na Taasisi wakimsikiliza
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bw. Cyrus
Kapinga (hayupo pichani) wakati akizindua Kambi ya Uchunguzi, Ushauri na Elimu
ya Afya uliofanyika katika jengo dogo la Ofisi hiyo Mji wa Serikali Mtumba
jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa,
Profesa Abel Makubi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI,
ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bw. Cyrus
Kapinga kuzindua Kambi
ya Uchunguzi, Ushauri na Elimu ya Afya uliofanyika katika jengo dogo la Ofisi
ya Rais-UTUMISHI Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bw. Cyrus Kapinga akipatiwa huduma ya kupimwa macho wakati wa uzinduzi wa Kambi ya Uchunguzi, Ushauri na Elimu ya Afya uliofanyika katika jengo dogo la Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa,
Profesa Abel Makubi (kushoto) akimkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bw. Cyrus
Kapinga kuzindua Kambi ya Uchunguzi, Ushauri na Elimu
ya Afya uliofanyika katika jengo dogo la Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mji wa Serikali
Mtumba jijini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu,
Hospitali ya Benjamin Mkapa, Bi. Prisca Lwangili.
Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu,
Bw. Musa Magufuli akitoa neno la shukrani kwa Viongozi na Watumishi wa Umma waliohudhuria
uzinduzi wa Kambi ya Uchunguzi, Ushauri na Elimu ya Afya
uliofanyika katika jengo dogo la Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mji wa Serikali Mtumba
jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi wa Umma wa Wizara
na Taasisi wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya kusikiliza hotuba ya Mwakilishi
wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya
Uendelezaji Sera, Bw. Cyrus Kapinga wakati wa uzinduzi
wa Kambi ya Uchunguzi, Ushauri na Elimu ya Afya uliofanyika katika jengo dogo
la Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU,
Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo
akitoa utambulisho wa Viongozi na wageni waliohudhuria uzinduzi
wa Kambi ya Uchunguzi, Ushauri na Elimu ya Afya uliofanyika katika jengo dogo la
Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyrus
Kapinga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Madaktari Bingwa kutoka
Hospitali ya Benjamin Mkapa wakati wa uzinduzi wa Kambi ya Uchunguzi, Ushauri
na Elimu ya Afya uliofanyika katika jengo dogo la Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mji wa
Serikali Mtumba jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment