Waziri wa Nchi, Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene ametoa rai kwa Waajiri na Viongozi wa Matawi ya TUGHE Tanzania kuhamasisha Watumishi wa Umma katika sehemu zao za kazi kujituma na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mhe.
Simbachawene ametoa rai hiyo wakati akifunga semina ya Waajiri na Viongozi wa
Matawi ya TUGHE iliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 Agosti, 2024 katika Hoteli
ya Lushgarden jijini Arusha.
Katika
hotuba yake alisitiza Waajiri na Viongozi hao kutafuta namna bora na kuishauri
Serikali ili kuweka utaratibu wa kuzuia watumishi wa umma kuingia kazini na
simu zao za mkononi kwa kuwa zimekuwa kikwazo kwa utoaji wa huduma bora kwa
umma.
“Nchi nyingine watumishi
hawatumii simu
wakiwa ofisini,
kazi yao ni kutoa huduma kwa umma, lakini
sisi tunachati tu badala
ya kufanya kazi. Piteni kwenye ofisi mbalimbali za umma muone
watumishi walivyobize na matumizi ya simu zao za mkononi tangu wanapoingia
kazini, mathalani mtumishi ana magrupu ya ‘WhatsApp’
zaidi ya ishirini na anasoma yote na kujibu, hivyo kutumia muda wa mwajiri kwa
manufaa binafsi. Ninawasihi muingilie kati na kuishi kaulimbiu yenu ya Huduma Bora, Maslahi Zaidi”.
Aliongeza kuwa,
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Mkuu wa Utumishi wa Umma anafanya
jitihada kubwa za kuboresha masilahi ya watumishi ikiwa ni pamoja na kuelekeza
kufanya maboresho ya kikokotoo,
kupandisha madaraja na mishahara, kulipa malimbikizo na kutoa ajira mpya kwa
lengo la kuboresha utumishi wa umma.
Aidha,
alibainisha kuwa wajibu wa msingi kwa mtumishi wa umma ni kuwahudumia wananchi
wakati wote ili waweze kufanya shughuli zao za kujenga taifa kwa urahisi, lakini
watumishi wamekuwa hawawajibiki ipasavyo na hivyo kuathiri mnyororo wa kuwatumikia wananchi.
Awali, Mwenyekiti
wa TUGHE Taifa Bw. Joel Kaminyoge amesema wameamua kuwakutanisha waajiri na
viongozi wa TUGHE kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya chama na waajiri
na zaidi kubainisha changomoto katika utumishi wa umma na kuzitafutia ufumbuzi
wa haraka.
Bw. Kaminyoge
amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa msikivu
wakati wote wanapowasilisha shida zao na kuzitafutia ufumbuzi haraka. Hivyo,
yeye na viongozi wenzake waliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika
utatuzi wa changamoto zinazojitokeza katika utumishi wa umma.
Halikadhalika, Katibu
wa Mkuu wa TUGHE Taifa Bw. Hery Mkunda aliongeza kwa kumshukuru Mhe.
Simbachawene kwa kutenga muda na kuitikia wito wa kuwa mgeni rasmi wakati wa
kufunga semina hiyo ambayo wamepata kujifunza masuala mbalimbali yenye manufaa
kwa washiriki na taifa kwa jumla.
Bw. Mkunda,
amewapongeza waajiri wote walioruhusu watumishi wao kushiriki semina hiyo na
amesema hawatajuta kuwaruhusu viongozi hao kwa kuwa wameongezeka thamani kutokana
na elimu iliyotolewa katika semina hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akitoa hatuba yake wakati wa kufunga Semina ya Waajiri na Viongozi wa Matawi ya TUGHE katika Hoteli ya Lushgarden jijini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wakifuatilia hatuba ya ufungaji wa Semina ya Waajiri na Viongozi wa Matawi ya TUGHE kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Hayupo pichani) katika Hoteli ya Lushgarden jijini Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akitoa cheti cha ushiriki wa Semina ya Waajiri na Viongozi wa Matawi ya TUGHE kwa Bw. John Mboya katika Hoteli ya Lushgarden jijini Arusha.
Mkurugenzi
Msaidizi -Idara ya Usimamizi wa Rasilimawatu Serikalini Bi. Jeanfrida Mshumbusi
akishiriki katika Semina ya Waajiri na Viongozi wa Matawi ya TUGHE iliyofanyika
katika Hoteli ya Lushgarden jijini Arusha tarehe 26 hadi 29 Agosti, 2024.
Baadhi
ya Washiriki wakifuatilia hatuba ya ufungaji wa Semina ya Waajiri na Viongozi
wa Matawi ya TUGHE kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Hayupo pichani) katika
Hoteli ya Lushgarden jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment