Monday, October 5, 2026

MHE. RIDHIWANI KIKWETE ASHUGHULIKIA KERO ZA WATUMISHI WA UMMA JIJINI TANGA

Na Veronica Mwafisi-Tanga

Tarehe 06 Oktoba, 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Tanga na kusikiliza changamoto wanazokutana nazo kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi kwa ustawi wa Utumishi wa Umma na maendeleo ya taifa.

Akizungumza na watumishi hao leo tarehe 06 Oktoba, 2026, Waziri Kikwete amesema kusikiliza kero na changamoto za Watumishi ni mojawapo ya jukumu lake akiwa ndiye Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Kikwete alitoa fursa kwa watumishi hao kuwasilisha changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa majukumu yao na alizifanyia kazi na zilizohitaji vielelezo aliwaelekeza watendaji wa Mkoa huo kuzitafutia ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

“Nimesikiliza changamoto zenu, zitaenda kufanyiwa kazi, tumpe muda Mkurugenzi huyu ni mgeni, ninaamini atazifanyia kazi kikamilifu,” Mhe. Kikwete ameongeza.


Waziri Kikwete ametoa wito kwa Waajiri wote kushughulikia changamoto zote za watumishi wanaowasimamia kwa wakati ikiwemo madai ya kupandishwa vyeo, madai ya uhamisho, na malimbikizo ya mishahara pamoja na madai mengine ya kiutumishi.

 

Aidha, kuhusu malimbikizo ya mishahara amesema Waajiri wanapaswa kuyahakiki madai hayo pamoja na kuweka viambatisho vyote muhimu vinavyohusiana na madai hayo kabla ya kuwasilisha Utumishi ili yahakikiwe na kuwasilishwa Hazina kwa ajili ya taratibu za malipo. “Mtumishi anapaswa kupata majibu ya changamoto alizonazo kwa wakati na kama lipo nje ya mamlaka ya mwajiri liwasilishwe katika Mamlaka inayofuata ili mtumishi apewe majibu.” Ameongeza


Amesema azma ya Mhe. Rais ya kuuboresha Utumishi wa Umma na Utawala Bora ilijidhihirisha rasmi wakati akilihutubia Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 14 Novemba, 2025, Mhe.Rais alisisitiza kuwa Serikali anayoingoza itaendeleza jitihada za kuimarisha maadili, nidhamu uzalendo, uwajibikaji pamoja na kusimamia haki na stahiki za Watumishi wa Umma na Watendaji mbalimbali serikalini ili kuongeza moyo wa kufanya kazi kwa bidii na uwajibikaji wa hiari kwenye Utumishi wa Umma.


“Kipekee niwaagize Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala kuwa viungo muhimu katika kuzishauri Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu katika kuhakikisha Haki na Wajibu za Watumishi wa Umma vinatolewa sambamba ili kuepusha malalamiko kwa watumishi wanaowasimamia.” Amesisitiza


Awali Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI aliwapongeza watumishi wa Mkoa wa Tanga kuwasilisha kero na changamoto zao kwa uhuru bila hofu.

“Nimefurahishwa sana, mnajitambua, mnapendana maana nimeona mnawasilisha changamoto zenu na hata kuzungumzia changamoto za wengine il zipatiwe ufumbuzi, huu ni upendo wa ajabu sana, hongereni,” ameongeza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa Umma jijini Tanga na kusikiliza kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi.

 


Sehemu ya Watumishi wa Umma jijini Tanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Ridhiwani Kikwete akitazama nyaraka zake wakati wa kikao chake na Watumishi wa Umma Mkoa wa Tanga kilicholenga  kusikiliza kero na changamoto zao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi.

 


Sehemu ya Watumishi wa Umma jijini Tanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao. 


Mtumishi kutoka jijini Tanga, Bw. Bakari Mkabala akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Ridhiwani Kikwete alipokuwa akisikiliza kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Ridhiwani Kikwete akifafanua baadhi ya hoja zilizowasilishwa wakati wa kikao kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi.


Mtumishi kutoka Shule ya Msingi Ummy Mwalimu, Bi. Amina Salehe  akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Ridhiwani Kikwete alipokuwa akisikiliza  kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi.



Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili akijibu moja ya hoja iliyowasilishwa  wakati wa kikao kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi.


Afisa Mtendaji wa Mtaa, jijini Tanga, Bw. Bakari Salim akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Ridhiwani Kikwete alipokuwa akisikiliza  kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi.


Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Mhe. Philimon Magesa akizungumza jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Ridhiwani Kikwete na Watumishi wa jiji hilo kilichofanyika kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za Watumishi wa Umma



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Ridhiwani Kikwete (kushoto) akisikiliza kero na changamoto mbalimbali za Watumishi wa Umma Mkoa wa Tanga. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili

Mtumishi kutoka jijini Tanga (aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Ridhiwani Kikwete alipokuwa akisikiliza  kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi.


Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mhe. Gilbert Kalima akifurahia jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) na watumishi wa Mkoa huo kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi.


Sehemu ya Watumishi wa Umma jijini Tanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao.


Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Mikanjuni, Bw. Peter Mpenzu akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Ridhiwani Kikwete alipokuwa akisikiliza  kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tanga Ufundi.



No comments:

Post a Comment