Monday, October 26, 2026

BI. LWANGILI AWATAKA WATUMISHI KUJITATHMINI KUIMARISHA MAHUSIANO NA UFANISI KAZINI

Na. Antonia Mbwambo-Dodoma

Tarehe 26 Oktoba, 2026

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili, amewataka watumishi wa Ofisi hiyo kujitathmini, kujitambua na kuelewa haiba za wenzao ili kuimarisha mahusiano na ushirikiano kazini kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Bi. Lwangili ameyasema hayo leo, Oktoba 26, 2026, wakati akihitimisha mafunzo kuhusu Haiba kwa watumishi wa Ofisi hiyo, yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

“Ni muhimu kwa kila mtumishi kujitathmini na kujifunza tabia za wengine ili kujenga mahusiano mazuri kazini, kuimarisha ushirikiano na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu,” amesema Bi. Lwangili.

Amesisitiza kuwa kujitambua na kuelewa haiba za wengine husaidia kurahisisha mawasiliano, kupunguza migogoro na kujenga mazingira bora ya kazi yanayozingatia kuheshimiana na kushirikiana.

Kwa upande wake, mwezeshaji ambaye ni Afisa kutoka Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Oswin Mkinga, amesema haiba ya mtumishi hujidhihirisha kupitia tabia, mwenendo, nidhamu, uadilifu, mawasiliano na namna anavyohusiana na wengine.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa watumishi kujitambua, kudhibiti hisia na kuheshimu maoni ya wengine ili kuimarisha mahusiano kazini, kuongeza ufanisi na kuboresha huduma kwa wananchi.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo wakati akihitimisha mafunzo kuhusu haiba yaliyotolewa na Afisa kutoka Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi Bw. Oswin Mkinga Oktoba, 26, 2026 jijini Dodoma


Baadhi ya wakurugenzi na watumishi kutoka Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifurahia jambo wakati wa mafunzo ya uelewa kuhusu haiba, yaliyotolewa na Afisa kutoka Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi Bw. Oswin Mkinga kwa watumishi wa Ofisi hiyo,  Oktoba 26, 2026 Mtumba Jijini Dodoma


Afisa kutoka Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Oswin Mkinga, akitoa mafunzo kuhusu haiba kwa watumishi wa Ofisi hiyo Oktoba 26,2026  katika eneo maalum la ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma

Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya uelewa kuhusu haiba, yaliyotolewa na Afisa Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi wa Ofisi hiyo Bw. Oswin Mkinga Oktoba 26, 2026 Mtumba jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo wakati akihitimisha mafunzo kuhusu haiba yaliyotolewa na Afisa kutoka Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi Bw. Oswin Mkinga Oktoba, 26, 2026 jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (wa pili kutoka kulia) akifurahia jambo wakati wa mafunzo ya uelewa kuhusu haiba, yaliyotolewa na Afisa kutoka Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi Bw. Oswin Mkinga kwa watumishi wa Ofisi hiyo,  Oktoba 26, 2026 Mtumba Jijini Dodoma.Wengine ni Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi hiyo.

Baadhi ya wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi. Prisca Lwangili (hayupo pichani) wakati akihitimisha mada kuhusu Haiba yaliyotolewa na Afisa kutoka Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi Bw. Oswin Mkinga Oktoba, 26, 2026 jijini Dodoma

Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifurahia jambo wakati wa mafunzo ya uelewa kuhusu haiba yaliyofanyika Oktoba 26, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma


Baadhi ya wakurugenzi na watumishi kutoka Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi. Prisca Lwangili (hayupo pichani) wakati akihitimisha mada kuhusu Haiba yaliyotolewa na Afisa kutoka Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi Bw. Oswin Mkinga Oktoba, 26, 2026 Mtumba jijini Dodoma

Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya uelewa kuhusu haiba, yaliyotolewa na Afisa Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi  wa Ofisi hiyo Bw. Oswin Mkinga Oktoba 26, 2026  Mtumba jijini Dodoma




Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Nyasinde Mukono akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya uelewa kuhusu haiba yaliyofanyika Oktoba 26, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo  Mtumba jijini Dodoma

Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya uelewa kuhusu haiba, yaliyotolewa na Afisa Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi  wa Ofisi hiyo Bw. Oswin Mkinga Oktoba 26, 2026  Mtumba jijini Dodoma


Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya uelewa kuhusu haiba, yaliyotolewa na Afisa Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi  wa Ofisi hiyo Bw. Oswin Mkinga Oktoba 26, 2026  Mtumba jijini Dodoma

Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya uelewa kuhusu haiba, yaliyotolewa na Afisa Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi  wa Ofisi hiyo Bw. Oswin Mkinga Oktoba 26, 2026  Mtumba jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo wakati akihitimisha mafunzo kuhusu haiba yaliyotolewa na Afisa kutoka Idara ya Usimamizi wa Utendajikazi Bw. Oswin Mkinga Oktoba, 26, 2026 jijini Dodoma


No comments:

Post a Comment