Friday, October 23, 2026

NAIBU WAZIRI QWARAY ASISITIZA MATUMIZI YA MFUMO WA E-UHAMISHO

Na Veronica Mwafisi-Lindi na Mtama

Tarehe 23 Oktoba, 2026

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amesema Serikali imeendelea kuimarisha mifumo ya kidijitali ili kuongeza uwazi, uwajibikaji, ufanisi na ubora wa huduma hiyo hivyo, Watumishi wa Umma wahakikishe katika maombi yao wanatumia Mfumo wa e-Uhamisho badala ya kuendelea kutegemea taratibu zinazoweza kusababisha urasimu na ucheleweshaji.

Naibu Waziri Qwaray amesema hayo leo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Umma wa maeneo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kusikiliza changamoto zinazowakabili Watumishi hao na kujadili namna bora ya kuimarisha utendaji.

Mhe. Qwaray amesema kuwa, maombi ya nakala ngumu yanayotumwa kwa Katibu Mkuu (UTUMISHI) hayatapokelewa badala yake njia sahihi ni kutumia mfumo huo wa e-Uhamisho.

Ameongeza kuwa, waajiri na wasimamizi wapitie maombi na kutoa maoni kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa ili kufanyia kazi kwa wakati kwani, maombi ya uhamisho kwa njia ya mfumo yana muda wa kukaa katika ofisi na yasipopitishwa ndani ya muda husika maombi hayo yataenda katika hatua inayofuata.

”Nitoe wito kwa waajiri na wasimamizi kupitia maombi na kutoa maoni kwa wakati kwani uhamisho kwa njia ya mfumo yana muda wake, kwa mkuu wa Taasisi ni siku 10, kwa msimamizi ni siku 4 na kwa mkuu wa Idara ni siku 3 yasipopitishwa kwa muda husika maombi haya yataenda katika hatua nyingine”, amesema Mhe. Qwaray

Akihitimisha hotuba yake Mhe, Qwaray amewataka Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kufanya kazi kwa bidii, kusimamia maadili na kuzingatia maslahi ya umma kwa lengo la kujenga imani ya Wananchi katika taasisi husika kwa ustawi wa Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Mhe. Qwaray amesema Wilaya ya Lindi inamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi ambazo zimesaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali  jambo ambalo linawapa ari Watumishi wa Umma ya kufanya kazi kwa moyo, upendo na kujituma.

Naye, Katibu Tawala Msaidizi, Utawala na Rasilimaliwatu-Lindi, Bw. Natalis Linuma amemshukuru Naibu Waziri, Mhe. Regina Qwaray kwa kufanya ziara katika Mkoa huo na kuahidi watatekeleza na kufanyia kazi maelekezo yote ambayo yametolewa kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na Watumishi wa Umma na kusikiliza kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

Sehemu ya Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi katika Halmashauri hiyo kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kushoto) akisikiliza hoja na changamoto zilizokuwa zikiwasilishwa na Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva


Afisa Muuguzi, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Bw, Paschal Petro akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akisikiliza kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi


Sehemu ya Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtama wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akifurahia jambo wakati wa kikao chake na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama (hawapo pichani) kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo  kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao.


Afisa Elimu kutoka Shule Maalum, Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, Bw. Hassan Nungu akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akisikiliza kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo.


Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva (aliyesimama) akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (wa kwanza kulia) kuzungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi 


Sehemu ya Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi katika Halmashauri hiyo kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (katikati) akifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakati wa kikao chake na Watumishi wa Umma hao kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva na wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omari.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akitazama nyaraka zake kabla ya kuzungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama wakati wa kikao chake na Watumishi hao kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao.


Sehemu ya Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtama wakifurahia jambo wakati Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akizungumza nao kwenye kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao.


Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati Naibu waziri huyo alipokuwa akizungumza nao kwenye kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto zao.


Afisa Mtendaji wa Kata, Halmashauri ya Wilaya ya Mtama , Bw. Msafiri Wanje akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akisikiliza kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo.


Afisa Mifugo Mwandamizi, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Bw. Gilya Ngwesa akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akisikiliza kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Katibu Tawala Msaidizi, Utawala na Rasilimaliwatu-Lindi, Bw. Natalis Linuma akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) mara baada ya Naibu Waziri huyo kuhitimisha ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi iliyolenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mara baada ya kuhitimisha kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi wa Umma.


Katibu wa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Faraja Maulidi akifuatilia jambo wakati wa kikao kazi cha  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manipaa ya Lindi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akipokea salamu kutoka kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa lengo la kufanya kikao cha kusikiliza kero na changamoto za Watumishi wa Umma.







No comments:

Post a Comment