Tuesday, October 6, 2026

WAZIRI KIKWETE AHITIMISHA MICHEZO YA SHIMIWI 2026, AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUJAZA PEPMIS NA KUSIMAMIA MIFUMO YA UTENDAJI KAZI

Na. Veronica Mwafisi-Moshi

07 Oktoba, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka Watumishi wa Umma waliokuwa katika michezo ya SHIMIWI watakaporudi katika maeneo yao ya kazi, kufanya kazi kwa kusimamia mifumo ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali waliyokasimiwa ikiwemo ujazaji wa Mfumo wa Upimaji wa Utendaji kazi (PEPMIS).

Waziri Kikwete amezungumza hayo leo tarehe 07 Oktoba, 2026 wakati akihitimisha rasmi michezo ya SHIMIWI iliyofanyika katika Mkoa wa Kilimanjaro.

“Nitoe wito kwenu watumishi wenzangu, leo tunapohitimisha rasmi michezo hii ya SHIMIWI, mtakaporudi katika maeneo yenu ya kazi  hakikisheni mnasimamia Mifumo ya utekelezaji wa majukumu yenu ikiwemo ujazaji wa PEPMIS,” amesema Mhe. Kikwete

Waziri Kikwete amesema, taasisi zote za Serikali zina utaratibu mzuri wa kumpima kila mtumishi kiutendaji hivyo, mafanikio ya mtu mmoja mmoja, Idara na taasisi kwa ujumla yatasaidia kujua utendaji wa Serikali nzima.

Ameongeza kuwa, ni vema kujenga ushirikiano kwa washiriki wa michezo hiyo ya SHIMIWI ambao utawasaidia katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika maeneo yao ya kazi.

“Mkusanyiko huu mkubwa wa Watumishi wa Umma unatusaidia kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali pamoja na kujenga ushirikiano utakaoleta mafanikio kwenye maeneo yenu ya kazi,” ameongeza Mhe. Kikwete

Aidha, Mhe. Ridhiwani amesisitiza suala la usimamizi wa Rasilimalifedha kwa Viongozi wa Klabu mbalimbali na kutaka kila ofisi kutenga bajeti kwa ajili ya mipango ya mwaka unaofuata.

Akihitimisha hotuba yake, Mhe. Ridhiwani amesema kutokana na Kaulimbiu ya SHIMIWI 2026, inayosema Watumishi Tupo Tayari kwa AFCON 2027, kila mtumishi katika sekta aliyopo ahakikishe anaunga mkono mashindano hayo kwa ustawi wa Taifa letu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa Umma wakati akifunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kushoto) akifurahia kuwakabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kombe la ushindi wa jumla mara baada ya Waziri huyo kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro. Aliyevaa koti jeusi ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili.


Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipokuwa akifunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Sehemu ya Watumishi wa Umma ambao ni wanamichezo kutoka katika Wizara mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipokuwa akifunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akimkabidhi kombe la mshindi wa kwanza kwa upande wa Netiboli Nahodha wa timu ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Elizabeth Fusi mara baada ya Waziri huyo kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akimkabidhi kombe la ushindi mmoja wa watumishi walioshinda mara baada ya Waziri huyo kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (kushoto) akifurahia mara baada ya timu ya netiboli kutoka Ofisi hiyo kupata kombe la ushindi wa kwanza kwa upande wa Netiboli wakati wa kufungwa Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa SHIMIWI, Bw. Daniel Mwalusamba  kabla ya Waziri huyo kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambao ni wanamichezo walioshiriki Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI)  wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kufunga mashindano hayo yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro


Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambao ni wanamichezo walioshiriki Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI)  wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kufunga mashindano hayo yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Chuo cha Polisi Tanzania (CCP MOSHI).


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) akifurahia jambo na Watendaji wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) na Viongozi mbalimbali kutoka katika Wizara mara baada ya Waziri huyo kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI)


Watumishi wa Umma kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakifurahia ushindi mara baada ya kukabidhiwa kombe la ushindi wakati wa kufungwa kwa Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa tatu kutoka kulia) akisikiliza maelezo ya awali kabla ya kushuhudia mchezo wa kuvuta kamba kabla ya Waziri huyo kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (aliyevaa koti jeusi) akifuatilia kwa umakini mchezo wa kuvuta kamba wakati wa Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro. Wa nne kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka katika Ofisi ya Rais-UTUMISHI. Wengine ni Wakurugenzi na Watumishi kutoka katika Wizara mbalimbali.


Viongozi na Watendaji wa Wizara na Taasisi mbalimbali wakishuhudia mchezo wa kuvuta kamba wakati wa Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kufunga mashindano hayo yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.











 

No comments:

Post a Comment