Sunday, October 4, 2026

UTUMISHI YAIGALAGAZA UJENZI 89–10 MPIRA WA PETE

 Na Eric Amani, Moshi

 

Timu ya mpira wa pete ya Utumishi imeendeleza kiwango chake bora katika Mashindano ya SHIMIWI 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 89–10 dhidi ya timu ya Ujenzi.

 

Oktoba 04, 2026 katika uwanja wa ushirika Utumishi ilianza mchezo huo kwa kasi na umakini, ikitawala maeneo mbalimbali ya uwanja na kutumia kwa ufanisi nafasi ilizopata katika eneo la ushambuliaji. Uwezo wa timu hiyo kujenga mashambulizi na kuyakamilisha kwa usahihi uliiwezesha kupata mabao mengi na kujenga tofauti kubwa dhidi ya Ujenzi.

 

Kadiri mchezo ulivyoendelea, Utumishi iliendelea kudhibiti mwelekeo wa mchezo, huku ikionyesha ushirikiano mzuri kati ya safu ya ulinzi na ushambuliaji. Ufanisi huo uliiwezesha timu hiyo kuongeza mabao na hatimaye kumaliza mchezo ikiwa mbele kwa mabao 89–10.

 

Ushindi huu unaendelea kuimarisha mwenendo wa Utumishi SC katika michuano hiyo, huku timu hiyo ikionyesha dhamira ya kufanya vizuri na kuendelea kupambana kuelekea mchezo wa fainali SHIMIWI 2026 dhidi ya Ikulu.

 

Mashindano hayo yanaendelea Moshi, mkoani Kilimanjaro, Umoja Kazini, Ushindi Uwanjani



No comments:

Post a Comment