Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 15 Oktoba, 2026
Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia taasisi yake ya Watumishi
Housing Investments (WHI) baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya ujenzi ya makazi kwa Watumishi wa Umma nchini.
Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Kamati hiyo mara baada ya
kuhitimisha ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi eneo la
Njedengwa na Mlezi jijini Dodoma leo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Edwin Swalle amesema ujenzi wa nyumba hizo unaakisi maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan ya kupeleka tabasamu kwa Watumishi wa Umma kwa kuwa
na uhakika wa makazi.
“Kwa niaba ya Kamati hii, nitoe pongezi kwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora kupitia WHI, nyumba 1500 zilizojengwa kwa ajili ya Watumishi wa Umma nchi nzima zitasaidia kupunguza
changamoto ya makazi kwa Watumishi wa Umma katika maeneo mengi nchini, kwa hakika mnafanya kazi nzuri ya kumwakilisha Mhe. Rais kwa kupeleka
tabasamu kwa Watumishi wa Umma ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wananchi.” Amesema Mhe. Swalle.
Aidha, Mhe. Swalle ameuelekeza uongozi wa WHI kuangalia namna ya kupata benki ya ardhi katika maeneo mengi
ili wajenge nyumba nyingi zaidi kwani watumishi wengi wana changamoto ya makazi
jambo ambalo hutishia watumishi hao kutaka kuhama.
“Watumishi wanaongezeka lakini ardhi haiongezeki, nashauri Ofisi
iweke kipaumbele kutafuta benki ya ardhi maeneo mbalimbali ili muwe na uhakika
wa kufanya miradi maeneo mbalimbali kutokana na uhitaji mkubwa wa nyumba za
watumishi.” Amesisitiza.
Kwa upande
wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema lengo la mradi huo ni kuongeza chachu ya utendaji kazi kwa Watumishi wa
Umma.
Amesema, WHI imeweka utaratibu wa namna ya kulipa fedha kwa wanaonunua nyumba hizo ili kuwapunguzia mzigo wa kulipa fedha nyingi kwa mkupuo kwa kuzingatia uwezo wao wa kifedha.
Katika hatua nyingine, Mhe. Ridhiwani amesema, Taasisi
hiyo ya WHI imeanzisha dirisha la e-wekeza kwenye mfumo wa Watumishi
Portal ambalo linawawezesha Watumishi wa Umma kuwekeza katika Mfuko wa Faida
(Faida Fund) kupitia makato ya hiari ya mshahara kila mwezi.
Mhe. Kikwete amesema, hatua hiyo imelenga kuwawezesha Watumishi wa Umma kujenga tabia ya kuwekeza na kuongeza uwezo wao wa kununua nyumba kabla na baada ya kustaafu. “Hivyo, e-wekeza ni hatua ya nyongeza ya uwezeshaji wa kifedha, sambamba na njia za kumiliki nyumba zinazotolewa na WHI,” ameongeza.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Waziri Kikwete, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray aliwashukuru wajumbe wa kamati hiyo kwa ushirikiano, miongozo na maelekezo ambayo wamekuwa wakitoa mara zote ambayo yamewezesha utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo pamoja na taasisi zake kwa ufasaha
Kwa niaba ya Waziri wake, Mhe. Qwaray ameiahidi kamati hiyo kuyafanyia kazi maoni, ushauri na maelekezo yote waliyoyatoa ili kuboresha utendaji kazi wa Ofisi hiyo pamoja na taasisi zake.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Bw. Sephania Solomon amesema fedha za ujenzi wa mradi wa Makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa utakamilishwa kwa wakati kama ilivyopangwa kwa awamu hiyo ya kwanza ambapo zinatarajiwa kukamilika mwezi February 2027.
Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Edwin Swale (kulia) akizungumza mara baada ya Kamati
yake kukagua utekelezaji mradi wa ujenzi wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo
la Njedengwa na Mlezi unaotekelezwa na Watumishi
Housing Investments (WHI) jijini Dodoma.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (aliyenyoosha kidole) akifafanua jambo kwa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji mradi wa ujenzi
wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa unaotekelezwa na Watumishi
Housing Investments (WHI) jijini Dodoma.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (kulia) akifafanua moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria baada ya Kamati hiyo
kukagua utekelezaji mradi wa ujenzi wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo
la Njedengwa na Mlezi unaotekelezwa na Watumishi Housing Investments (WHI)
jijini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Edwin Swale
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Utawala, Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akielezea utekelezaji mradi wa ujenzi wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa na
Mlezi unaotekelezwa na Watumishi Housing Investments (WHI) jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa maelezo ya awali kabla ya
kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria, Mhe. Edwin
Swale kuzungumza na WViongozi na watendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI)
mara baada ya Kamati hiyo kukagua utekelezaji mradi wa ujenzi wa
makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa na Mlezi jijini Dodoma.
Naibu Waziri. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akitoa neno la shukrani kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria baada ya Kamati hiyo kutembelea na kukagua utekelezaji mradi wa ujenzi wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa na Mlezi unaotekelezwa na Watumishi Housing Investments (WHI) jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na
Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa
Idara ya Mipango wa Ofisi hiyo Bw. Cosmas Ngangaji (kulia) kabla ya Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kuwasili kwa ajili ya kukagua utekelezaji
wa mradi wa ujenzi wa makazi kwa Watumishi
wa Umma eneo la Njedengwa unaotekelezwa na Watumishi Housing Investments (WHI)
jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Bw.
Sephania Solomon (wa kwanza kulia) akisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa
zikiwasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria mara baada ya Kamati hiyo kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa na
Mlezi unaotekelezwa na Watumishi Housing Investments (WHI) jijini Dodoma.
Mjumbe
wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Oscar
Kikoyo akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya Kamati hiyo kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa
makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa na Mlezi unaotekelezwa na
Watumishi Housing Investments (WHI) jijini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya
Rais-UTUMISHI wakifuatilia hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Edwin
Swale alipokuwa akizungumza mara baada ya Kamati yake kukagua utekelezaji
mradi wa ujenzi wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa na
Mlezi unaotekelezwa na Watumishi Housing Investments (WHI) jijini Dodoma.
Sehemu ya
Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia
hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria, Mhe. Edwin Swale alipokuwa
akizungumza mara baada ya Kamati yake kukagua utekelezaji mradi wa ujenzi
wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa na Mlezi unaotekelezwa na
Watumishi Housing Investments (WHI) jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Edwin Swale (katikati) akifuatilia jambo mara baada ya Kamati
yake kukagua utekelezaji mradi wa ujenzi wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo
la Njedengwa na Mlezi unaotekelezwa na Watumishi Housing Investments (WHI)
jijini Dodoma. Wengine ni Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Bw.
Sephania Solomon (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete (wa pili kutoka kushoto) kabla ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala, Katiba na Sheria kuwasili katika eneo hilo kukagua utekelezaji mradi wa ujenzi wa makazi kwa Watumishi wa Umma Njedengwa. Wengine ni
Viongozi wa Ofisi hiyo.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bi. Mary Mwakapenda akifuatilia jambo wakati Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Edwin Swale (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza mara baada ya Kamati yake kukagua utekelezaji mradi wa ujenzi wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa na
Mlezi unaotekelezwa na Watumishi Housing Investments (WHI) jijini Dodoma.
Sehemu ya
Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia
hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria, Mhe. Edwin Swale alipokuwa
akizungumza mara baada ya Kamati yake kukagua utekelezaji mradi wa ujenzi
wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa na Mlezi unaotekelezwa na
Watumishi Housing Investments (WHI) jijini Dodoma.
Sehemu ya
Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia
hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria, Mhe. Edwin Swale alipokuwa
akizungumza mara baada ya Kamati yake kukagua utekelezaji mradi wa ujenzi
wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa na Mlezi unaotekelezwa na
Watumishi Housing Investments (WHI) jijini Dodoma.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyenyanyua mikono) akifafanua jambo kwa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji mradi wa ujenzi
wa makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa unaotekelezwa na Watumishi
Housing Investments (WHI) jijini Dodoma.
Muonekano wa jengo la nyumba za Watumishi wa Umma lililopo eneo
la Njedengwa mkoani Dodoma ambalo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria walitembelea na kukagua utekelezaji wa mradi
wa ujenzi huo.







No comments:
Post a Comment