Veronica Mwafisi-Moshi
Tarehe 08 Oktoba, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa mstari wa mbele kulinda heshima ya chombo hicho nyeti na hatimaye watakapotoka hapo wawe tayari kulitumikia Taifa katika misingi ya maadili na uzalendo.
Mhe. Kikwete amesema hayo leo tarehe 8 Oktoba, 2026 wakati akifungua mafunzo ya awali ya Uchunguzi kwa vijana hao yanayofanyika katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi.
“Tambueni kwamba, TAKUKURU ni chombo nyeti sana na cha kiuchunguzi kinachosimamia maadili, hivyo mna wajibu wa kuhakikisha mnakuwa mstari wa mbele kulinda heshima yake,” amesisitiza.
Amesema Serikali inatambua umuhimu wa Mafunzo hayo ya awali ya Uchunguzi katika kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa Uadilifu na Ueledi Mkubwa. “Hivyo ni matarajio yangu na ya Serikali kwa ujumla kuwa, mtatilia maanani na kwa uzito unaotakiwa mafunzo haya, ili mkitoka hapa mkawe mabalozi wema wa TAKUKURU katika vituo mtakavyopangiwa kwenda kufanya kazi” ameongeza.
Amewasisitiza kufuata miongozo, maelekezo pamoja na taratibu zote zitakazotolewa wakati wote watakapokuwa katika mafunzo pamoja na kuzingatia kila wanachofundishwa kwa umakini mkubwa kwakuwa ndicho kitakachoamua hatma ya ajira ya kila mmoja wao ndani ya TAKUKURU.
Waziri Kikwete amewapongeza vijana hao kwa kufanikiwa kuitwa katika hatua hiyo ya mwisho ya Mchakato wa Ajira wa Taasisi kwani ushindani ulikuwa ni mkubwa sana.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila akiwasilisha taarifa ya utendaji wa TAKUKURU alisema mafunzo hayo ni sharti la kimuundo, hivyo kila anayeajiriwa TAKUKURU ni lazima ashiriki kwani yanawasaidia kupata ujuzi na utalaam wa kuzuia na kupambana na rushwa.
Amesema mafunzo hayo yalianza tarehe 19 Septemba
2026 na yatafanyika kwa muda wa miezi mitano ambapo yataendeshwa kwa njia ya
vitendo na nadharia ikiwemo kufundishwa suala la maadili katika Utumishi wa
Umma na ajira itatolewa baada ya kuhitimu na kufaulu mitihani itakayotolewa
wakati wa mafunzo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati akifungua mafunzo hayo katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi.
Sehemu ya vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akifungua mafunzo hayo katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi.
Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila akielezea
lengo la mafunzo ya vijana wanaofanya mafunzo
ya awali ya Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kufungua mafunzo hayo.
Sehemu ya vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akifungua mafunzo hayo katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi.
Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma - Ofisi ya Rais, UTUMISHI, SACP Ibrahim
Mahumi akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akifungua mafunzo kwa vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika Shule
ya Polisi Tanzania-Moshi.
Wakurugenzi, Watendaji wa taasisi mbalimbali na maafisa wa vyombo vya
ulinzi na usalama wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete alipokuwa akifungua mafunzo kwa vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika Shule
ya Polisi Tanzania-Moshi.
Sehemu ya vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akifungua mafunzo hayo katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bi Neema Mwakalyelye mara baada ya Waziri huyo kuwasili katika Shule ya
Polisi Tanzania-Moshi kufungua mafunzo ya vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya
Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo kabla ya kufungua mafunzo ya vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi.
Wakurugenzi, Watendaji wa taasisi mbalimbali, maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama na vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akifungua mafunzo kwa vijana hao katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kushoto) akiwasili katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi kufungua mafunzo kwa vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila.
Watendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akifungua kwa vijana mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya TAKUKURU
Sehemu ya vijana wanaofanya mafunzo ya
awali ya Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete wakati akifungua mafunzo hayo katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wakufunzi wa Shule ya Polisi Tanzania-Moshi (waliosimama) mara baada ya Waziri huyo kufungua kwa vijana mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mara baada ya Waziri huyo kufungua mafunzo hayo katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na
Watendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) mara baada ya Waziri huyo kufungua mafunzo kwa vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya
TAKUKURU katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi.
















No comments:
Post a Comment