Veronica Mwafisi-Tanga
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekagua maendeleo ya ujenzi wa wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Tanga na kuupongeza uongozi wa chuo hicho kwa usimamizi mzuri.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi huo, Mhe. Kikwete amesema anafarijika na hatua nzuri aliyoiona ya ujenzi huo. “Sisi ndani ya Serikali tunajua umuhimu wa jengo hili, sio pambo bali tunataka kuona majengo haya yanakuwa kitovu cha kutoa elimu katika Mkoa huu wa Tanga.” Mhe. Kikwete ameongeza.
Amesema ni matamanio ya Serikali kuona ujenzi huo unakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa ili kufikia malengo yaliyowekwa. “Natamani kuona mwezi Mei 2027 jengo liwe limekamilika na kuanza kutumika ili pia tuweze kuendelea na ujenzi wa majengo mengine ndani ya Kampasi hii.” Amesema Mhe. Kikwete.
Amemsihi Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi kuendelea kuifanya kazi hiyo vizuri zaidi ili kukwepa kadhia ya kubadilisha Mkandarasi mwingine pale ambapo watashindwa kufanya kama ilivyofikiwa.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Kikwete kuzungumza, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mhe. Gilbert Kalima aliishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma katika mkoa huo.
Naye Kaimu Katibu Mkuu-UTUMISHI ambaye pia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi. Prisca Lwangili amemshukuru Waziri Ridhiwani kwa
mipango mizuri na namna anavyofanya ufuatiliaji wa mambo mbalimbali ikiwemo
maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho.
Akiwasilisha taarifa fupi ya maendeleo ya mradi wa ujenzi huo, Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Ernest Mabonesho amesema ujenzi wa chuo hicho ukikamilika unatarajiwa kuchukua jumla ya wanafunzi 2,000.
Dkt. Mabonesha amemshukuru Mhe. Kikwete kwa kufanya
ufuatiliaji wa mara kwa mara na kuwahimiza utekelezaji wa majukumu yao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC)
Mkoa wa Tanga mara baada ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi
wa Chuo hicho kilichopo Kata ya Maweni, Kange mkoani Tanga.
Kaimu Katibu Mkuu-UTUMISHI ambaye ni Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili akitoa maelezo ya awali kabla
ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa kwanza
kushoto) kuzungumza na Viongozi Watumishi wa
Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) Mkoa wa Tanga
mara baada ya Waziri huyo kukagua
maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo hicho kilichopo Kata ya Maweni, Kange mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa
pili kutoka kushoto) akipata maelezo ya mradi wa
ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) ulipofikia wakati alipotembelea
mradi huo uliopo Kata ya Maweni, Kange mkoani Tanga.
Mkurugenzi wa Kampasi ya Tanga ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Bi.
Zawadi Rashid akitoa neno la shukrani kwa Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) mara baada ya Waziri huyo kukagua maendeleo
ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa chuo hicho
kilichopo Kampasi ya Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akijadili jambo na Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt.
Ernest Mabonesho (kulia) mara baada ya Waziri huyo kukagua
maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kilichopo Kampasi ya Tanga.
Sehemu ya Wataalam wa ujenzi
wanaojenga Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kilichopo Kampasi ya Tanga
wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukagua maendeleo ya utekelezaji
wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kilichopo Kampasi ya Tanga.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (aliyenyoosha mkono) akisisitiza
jambo wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma (TPSC) kilichopo Kata ya Maweni, Kange mkoani Tanga.
Sehemu ya Wataalam wa ujenzi wanaojenga Chuo cha Utumishi wa Umma
(TPSC) kilichopo Kampasi ya Tanga wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukagua maendeleo ya utekelezaji
wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kilichopo Kampasi ya Tanga.
Mwonekano wa jengo la mradi wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) Kampasi ya Tanga.










No comments:
Post a Comment