Na Veronica Mwafisi-Kilwa
Tarehe 21 Oktoba, 2026
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amesema Watumishi wa Umma ni miongoni mwa nguzo kuu ya kufanikisha malengo ya taifa hivyo, katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni vema kila mtumishi akaongeza tija, kuboresha utendaji na kuhakikisha mipango ya Serikali inatafsiriwa kwa huduma na matokeo yanayoonekana katika maisha ya wananchi.
Mhe. Naibu Waziri Qwaray ameyasema hayo leo tarehe 21 Oktoba, 2026 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko wakati akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.
Mhe. Qwaray amesema, lengo la ziara hiyo ni kusikiliza changamoto zinazowakabili Watumishi hao na kujadili namna bora ya kuimarisha utendaji kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Naibu Waziri Qwaray alitoa fursa kwa watumishi hao na kusikiliza changamoto na hoja mbalimbali zinazokwamisha utekelezaji wa majukumu yao ambapo baadhi alizifanyia kazi na nyingine alizielekeza kwa Maafisa Utumishi wa Halmashauri hiyo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa haraka.
Vilevile Naibu Waziri Qwaray amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua kuwa ili kufikia uchumi wa kipato cha kati cha juu ni wajibu wa Watumishi hao kuongeza kasi ya utendaji, kutumia teknolojia ipasavyo na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma stahiki kwa wakati, kwa haki na bila usumbufu.
Akihitimisha hotuba yake wakati akizungumza na Watumishi hao Mhe. Qwaray amesema, Utumishi wa Umma ni dhamana hivyo, kila mmoja awajibike katika kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, taratibu, weledi na maslahi mapana ya Taifa.
Kwa upande wake Katibu
Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omari ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha nyingi kwa ajili ya
kutekeleza Miradi ya Maendeleo ikiwemo majengo ya kutolea huduma mbalimbali za afya, shule, nyumba za watumishi, majengo ya utawala
pamoja na miundombinu jambo ambalo linawapa ari ya utendaji kazi Watumishi wa Halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na Watumishi wa
Umma na kusikiliza kero na changamoto
zao wakati wa kikao kilichofanyika katika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa
Masoko, Halmashauri
ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.
Sehemu ya Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa
akizungumza nao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha
Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akiteta jambo na Katibu Tawala
Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omari (kushoto) wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha
Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za
Watumishi wa Umma.
Sehemu ya Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri
ya Wilaya ya Kilwa wakipiga makofi mara baada ya Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray
kuhitimisha hotuba yake wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha
Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko, kilicholenga
kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao.
Sehemu ya Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri
ya Wilaya ya Kilwa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa
akizungumza nao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko, kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za
Watumishi hao.
Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omari akitoa
maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kuzungumza na Watumishi
wa Umma wa Halmashauri
ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi wakati wa
kikao kilichofanyika katika kwenye
Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko kilicholenga kusikiliza kero na changamoto zao.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Kikanda, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Mpumbiye Mpumbiye akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akisikiliza kero na changamoto zao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko.
Mtumishi wa Umma kutoka
Idara ya Kilimo, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Bw. Maulid Kikali akiwasilisha
hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akisikiliza kero na changamoto zao wakati
wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo
ya Wananchi Kilwa Masoko.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Regina Qwaray (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati
ya Ulinzi na Usalama katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mara baada ya Naibu
Waziri huyo kuzungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri hiyo wakati wa kikao
kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Regina Qwaray (katikati) akiteta jambo na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kilwa wakati wa kikao cha Naibu Waziri huyo na Watumishi wa Umma wa Halmashauri
hiyo kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao.
Sehemu ya Watumishi wa Umma
kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Kilwa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko, kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao.
Katibu Tawala wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Bw. Yusuph Mrisho (aliyesimama kushoto) akizungumza
jambo wakati wa kikao cha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (wa kwanza
kulia) kilicholenga kuzungumza na Watumishi wa Halmashauri hiyo kilichofanyika
kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto zao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Sehemu ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mara baada ya Naibu Waziri huyo kuzungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri hiyo wakati wa kikao kilicholenga kusikiliza kero na changamoto za Watumishi hao.
Afisa Utumishi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Bw. Msena Bina akijibu moja ya hoja aliyoelekezwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) kuijibu kwa Mtumishi aliyewasilisha hoja hiyo wakati wa kikao cha Naibu Waziri huyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Regina Qwaray (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Sehemu ya Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mara baada ya Naibu Waziri huyo kuzungumza na Watumishi wa Umma wa
Halmashauri hiyo wakati wa kikao kilicholenga kusikiliza
kero na changamoto za Watumishi hao.














No comments:
Post a Comment