Tuesday, March 24, 2026

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE  YAMPONGEZA RAIS MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUWEKA KIPAUMBELE KWENYE SUALA LA AJIRA

Na. Antonia Mbwambo-Dodoma

Tarehe 24 Machi, 2026 

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kulipa kipaumbele suala la ajira katika utumishi wa umma. 

Pongezi hizo zimetolewa leo Machi 24, 2026 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Edwin Swalle wakati akimwakilisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo katika kikao cha  kupokea Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2026/27  kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma .

Amesema kasi ya kutoa vibali vya ajira kwa sasa imekuwa ni kubwa na ya kuridhisha ukilinganisha na miaka iliyopita. “Kwa niaba ya Kamati nipende kutoa pongezi nyingi kwa Mhe. Rais kwa kutoa vibali vya ajira pamoja na wewe Mhe. Waziri Kikwete na wasaidizi wote kwa utekelezaji kwani tumeona msukumo mkubwa kwenye suala la ajira katika Serikali hii ya Awamu ya Sita, hongereni sana,” ameongeza Mhe. Swalle.

Aidha, amewapongeza Viongozi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa ushirikiano kwa kamati hiyo ambao umerahisisha utekelezaji wa majukumu ya kamati.

“Mhe. Waziri Kikwete umekuwa ukitupatia ushirikiano mkubwa sana katika utekelezaji wa majukumu yetu, wewe pamoja watendaji wote wa Ofisi hii, mmefanya kazi yetu kuwa rahisi sana, hata katika ziara ya kamati tuliyoifanya Kanda ya Ziwa hivi karibuni hukuwahi kutuacha, ulikuwa nasi bega kwa bega, tunakupongeza kwa kuonyesha uko makini sana na kazi yako,” ameongeza Mhe. Swalle.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema, Ofisi yake ipo tayari kutoa ushirikiano wowote unaohitajika katika kufanikisha utekelekezaji wa majukumu ya kamati ili kuweza kufikia malengo iliyojiwekea katika kuhudumia wananchi. 





Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Mhe. Edwin Swalle akitoa neno la pongezi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa utendaji mzuri wa Ofisi yake katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria kilicholenga kupokea utekelezaji wa bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma  

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma  


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani)  wakati akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria kilicholenga kupokea utekelezaji wa bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa neno la shukrani kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria kwa kupokea na kujadili kwa kina kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 jijini Dodoma.

Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kuwasilisha utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma




Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kuwasilisha utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria kilicholenga kupokea utekelezaji wa bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa neno la shukrani kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria kwa kupokea na kujadili kwa kina kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe.Nyamizi Mhoja (aliyekaa katikati) akitaka ufafanuzi wa jambo baada ya wasilisho la utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe.Dkt Yahaya Nawanda akitaka ufafanuzi wa jambo baada ya wasilisho la utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma 

Katibu Mkuu Ikulu Bw. Mululi Mahendeka (kulia) akiteta jambo na  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Xavier Daudi (kushoto) wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria,kilicholenga kupokea utekelezaji wa bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma 

Mkurugenzi wa Mipango kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji akitoa Ufafanuzi wa jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, wakati wa kikao cha kupokea utekelezaji wa bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma 

 

Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani)  wakati akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Mick Kiliba akitoa maelezo ya jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, wakati wa kikao cha kupokea utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma 

Sehemu ya Wakurugenzi na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani)  wakati akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma

 

Sehemu ya wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani)  wakati akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma 


No comments:

Post a Comment