Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 16 Machi, 2026
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi ameielekeza
Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ya Ofisi hiyo kuendeleza
programu ya mafunzo kwa Watumishi wa Umma kila Jumatatu ya wiki kupitia
wataalamu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Ofisi hiyo ili kuwajengea uwezo
watumishi katika utekelezaji wa majukumu yao utakaosababisha Ufanisi katika utoaji
wa huduma na kuleta tija kwa jamii.
Bw. Daudi ameyasema hayo Machi
16, 2026 wakati akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala
Bora alipokuwa akihitimisha programu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi hao jijini Dodoma.
“Nipende
kuwapongeza watumishi wenzetu walioendesha mada mbalimbali katika programu hii
ya mafunzo kwa weledi, ujasiri, na umahiri mkubwa ili kuhakikisha uelewa
unajengeka kwa watumishi wa umma na kuimarisha utendaji kazi kwa maslahi ya
Taifa”. Bw. Daudi alisema
Aidha,
amewasisitiza watumishi wa Ofisi yake kuutumia utaalamu walionao na uwezo wanaojengewa
mara kwa mara kutekeleza majukumu yao kwa juhudi na ufanisi ili kutoa huduma
bora na kwa wakati kwa wananchi.
Naye
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, SACP. Ibrahimu Mahumi amesema Ofisi ya Rais-UTUMISHI imeanzisha
utaratibu wa kushirikishana uzoefu wa kitaalamu kwa watumishi wengine kwa kila Idara
kupitia programu ya mafunzo ya kila wiki ili kujenga uelewa mpana utakaosababisha
umahiri katika utendaji kazi.
Akiwasilisha
mada inayohusiana na masuala ya Uhamisho katika Utumishi wa Umma, Afisa
Utumishi Mwandamizi, kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Bw. Said Ally amesema lengo la kushirikishana uzoefu kwa
wataalamu wa ndani ni kuhakikisha kila mtumishi ndani ya Ofisi hiyo anakuwa na
uelewa utakaomuwezesha kuyajua majukumu ya kila Idara ili kutoa huduma kwa
wananchi kwa uharaka na ubora zaidi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi
Msaidizi, Sehemu ya Sera za TEHAMA na Viwango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw.
Ibrahim Toure, akiwasilisha mada ya Usalama Mtandaoni, amesema lengo la mada
hiyo ni kukumbushana juu ya matumizi sahihi ya mifumo ili kuwa na mtazamo na utamaduni
wa usalama mtandaoni wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku na hata
wawapo nje ya Ofisi.
Vilevile
Afisa TEHAMA Mkuu, Idara ya TEHAMA Serikalini, Bi. Zalika Hussein amesema elimu
ya usalama mtandaoni itawawezesha watumishi kuhakikisha mifumo na
miundombinu ya TEHAMA na taarifa zinazohifadhiwa kwenye mifumo hiyo zinakuwa
salama bila kufikiwa na watu wasiohusika kwa kuhakikisha wanatumia nywila zao wenyewe bila kumshirikisha
mtu mwingine yeyote kwa lengo la kulinda taarifa za serikali ikiwa ni utaratibu wa kuhakikisha usalama, usiri, na
uadilifu wa data za umma dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo wakati
akihitimisha programu ya mafunzo ya
kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi hao leo tarehe 16 Machi, 2026 jijini
Dodoma
Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, SACP. Ibrahimu Mahumi akiwaelimisha watumishi wa Ofisi
hiyo kuhusu umuhimu wa kushirikishana uzoefu wa kitaaluma katika kuleta ufanisi
wa kazi wakati wa mafunzo ya kuwajengea watumishi hao uwezo wa kiutendaji
yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi
wa umma kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) akizungumza nao wakati akihitimisha
programu ya mafunzo ya kuwajengea
uwezo wa kiutendaji Watumishi hao jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Sera za Tehama na
Viwango, Ofisi ya Rais- ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Itawala
Bora, Bw. Ibrahim Toure, akiwasilisha mada ya Usalama Mtandaoni wakati wa
mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa Ofisi hiyo machi 16,
2026 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (kushoto) pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa
Ofisi hiyo wakifuatilia mafunzo maalumu ambayo hufanyika kila wiki kwa lengo la
kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi
wa umma kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) akizungumza nao wakati akihitimisha
programu ya mafunzo ya kuwajengea
uwezo wa kiutendaji Watumishi hao jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa umma kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) akizungumza nao wakati akihitimisha programu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi hao jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa umma kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) akizungumza nao wakati akihitimisha programu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi hao jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment