Monday, March 30, 2026

WATUMISHI WA UMMA WAHIMIZWA KUONGEZA UWAJIBIKAJI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 30 Machi, 2026.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma                                                                                                                                     na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amewahimiza Watumishi wa Umma kuongeza uwajibikaji katika kuwahudumia wananchi.

Bw. Daudi ametoa wito huo leo alipokuwa akiwapongeza Watumishi wa Ofisi hiyo waliozaliwa mwezi Machi, 2026 mara baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo yanayofanyika kila siku ya Jumatatu Mtumba Jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi watumishi wa ofisi hiyo.

Bw. Daudi amesema, mtumishi wa umma anapoongeza umri imsaidie kuongeza chachu ya utendajikazi ili kutimiza malengo ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

''Nitoe wito kwa Watumishi wa Umma mnapoongeza umri na kusherehekea siku yenu ya kuzaliwa, hakikisheni mnawajibika ipasavyo katika maeneo yenu ya kazi hasa mnapotoa huduma kwa Watumishi wa Umma wenzenu na Wananchi, hakikisheni kuwa mnatimiza malengo ya Serikali katika kutoa huduma bora kwa kila Mtanzania.” amesema Bw. Daudi.


Awali katika mafunzo hayo, Afisa Rasilimaliwatu Mkuu kutoka katika ofisi hiyo, Idara ya Mishahara, Maslahi na Marupurupu, Bi. Magreth Banogile akiwasilisha mada kuhusu Motisha katika Utumishi wa Umma alisema, motisha ni manufaa anayoyapata mtumishi baada ya mshahara kutokana na majukumu anayoyatekeleza hivyo ni wajibu wa kila mtumishi wa umma kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili aweze kupata stahiki ya motisha husika.

Ameongeza kuwa baadhi ya motisha katika Utumishi wa Umma ni pamoja na mazingira bora ya kazi, vitendea kazi, fursa za mafunzo, huduma ya usafiri wa kwenda na kurudi kutoka kazini, pamoja na fursa ya muda wa kufanya mazoezi.

Aidha, katika mafunzo hayo kulikuwa na mada mbalimbali zilizowasilishwa na Maafisa kutoka katika Idara hiyo ya Mishahara, Maslahi na Marupurupu ambapo Afisa Rasilimaliwatu Mwandamizi Bw. Baraka Kilagu aliwasilisha mada kuhusu Miundo ya Maendeleo ya Utumishi chini ya Wizara pamoja na Afisa Rasilimaliwatu Mwandamizi, Bw. Imani Mtumbi aliyewasilisha mada kuhusu Miundo ya Mishahara katika Utumishi wa Umma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa ofisi hiyo waliokuwa wakiadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwao mwezi Machi, 2026. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Musa Magufuli.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akifurahia jambo alipokuwa akizungumza na Watumishi wa ofisi hiyo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yanayofanyika kila Jumatatu kwenye Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia wasilisho la mada kuhusu Miundo ya Maendeleo ya Utumishi chini ya Wizara wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika ofisi hiyo jijini Dodoma.


Afisa Rasilimaliwatu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Idara ya Mishahara, Maslahi na Marupurupu, Bw. Baraka Kilagu (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu Miundo ya Maendeleo ya Utumishi chini ya Wizara wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika ofisi hiyo jijini Dodoma. Waliokaa wa kwanza kulia ni Afisa Rasilimaliwatu Mkuu kutoka ofisi hiyo Bi. Magreth Banogile na katikati ni Afisa Rasilimaliwatu Mwandamizi, Bw. Imani Mtumbi


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia wasilisho la mada kuhusu Miundo ya Mishahara katika Utumishi wa Umma wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo ambayo hufanyika katika ofisi hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia wasilisho la mada kuhusu Miundo ya Mishahara katika Utumishi wa Umma wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo ambayo hufanyika katika ofisi hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika ofisi hiyo jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Musa Magufuli (aliyesimama) akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi kuzungumza na Watumishi wa ofisi hiyo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji yaliyofanyika katika ofisi hiyo jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia wasilisho la mada kuhusu Miundo ya Mishahara katika Utumishi wa Umma wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo ambayo hufanyika katika ofisi hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Mhasibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Tumwimbilege Ilomo akikata keki kwa niaba ya Watumishi wa ofisi hiyo wanaoadhimisha  kumbukizi ya kuzaliwa kwao mwezi Machi, 2026.


Mhasibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Tumwimbilege Ilomo (kulia) akimlisha keki Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili, Bi. Felister Shuli (kushoto) kwa niaba ya Watumishi wote waliozaliwa Mwezi Machi, 2026.






No comments:

Post a Comment