Friday, March 27, 2026

KATIBU MKUU MKOMI AWATAKA WADAU WA RASILIMALIWATU KATIKA SEKTA YA UMMA KUPENDEKEZA MKAKATI MADHUBUTI WA SULUHISHO LA UPUNGUFU WA WATUMISHI

 Na. Antonia Mbwambo na Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 27 Machi, 2026.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw, Juma Mkomi amewataka wadau wa Rasilimaliwatu Serikalini kupendekeza mkakati madhubuti utakaosaidia kuepukana na changamoto ya upungufu wa watumishi katika taasisi za umma.

Katibu Mkuu Mkomi ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka katika Wizara na Taasisi za Kimkakati kilicholenga kujadili matokeo ya tathmini ya mahitaji ya rasilimaliwatu.

Amesema Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ilifanya zoezi la Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika taasisi za umma na kubaini kuwepo kwa upungufu wa watumishi kwenye baadhi ya taasisi na taasisi nyingine kuwepo kwa ziada ya watumishi.

Amesema kufuatia tathmni hiyo, Ofisi iliona ni vema ikaandaa kikao cha wadau hao ili kujadiliana kwa pamoja namna itakavyofaa kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo ya muda mrefu.

Amesema kila mwaka wakati wa bajeti taasisi za umma zimekuwa na utaratibu wa kuomba watumishi, hivyo mkakati madhubuti uwekwe ili kupata suluhisho la changamoto hiyo ya upungufu wa watumishi.

“Lengo kubwa la kikao kazi hiki ni kupata usahihi wa taarifa za watumishi au mahitaji ya watumishi katika taasisi za umma, kuna maeneo yanahitaji watumishi kimkakati hivyo ni muhimu kuona namna ya kukubaliana katika kuwapata watumishi hao na kujadiliana kwa kina ili kupata mapendekezo yatakayosaidia kuwagawa Watumishi wa ajira mpya na watakaokuwa wakihamia katika vituo vingine vya kazi,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda amesema kupitia kikao kazi hicho Serikali itapata taarifa zilizo sahihi  za mahitaji ya Watumishi wa Umma kwa miaka mitano ijayo.

Akitoa neno la shukrani Mwenyekiti wa Kikao kazi hicho ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Wizara ya Afya, Bw. Issa Ng’imba alimuahidi Katibu Mkuu Mkomi kuwa watazingatia maelekezo yote ambayo ameyatoa ili waweze kuboresha utendaji kazi kwa maendeleo ya Taifa

 


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi akizungumza na washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu (hawapo pichani) kilicholenga kujadili matokeo ya tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Sekta na Taasisi za kimkakati kabla ya Katibu huyo kufungua kikao hicho kilichofanyika Machi 27, 2026 katika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi kutoka Idara na Vitengo vya Ofisi hiyo mara baada ya Katibu huyo kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kilichofanyika Machi 27, 2026 katika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Nishati Bi. Bahati Mtono akitaka ufafanuzi wa jambo wakati wa majadiliano ya mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kilicholenga kujadili matokeo ya tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Sekta na Taasisi za kimkakati kilichofanyika kilichofanyika Machi 27, 2026 katika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma

Wajumbe wa Sekretarieti kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kilicholenga kujadili matokeo ya tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Sekta na Taasisi za kimkakati kilichofanyika kilichofanyika Machi 27, 2026 katika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma.

Afisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Waziri Mkumbo akiwasilisha mada ya Mfumo wa e-Msawazo na matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Sekta na Taasisi za Kimkakati wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kilicholenga kujadili matokeo ya tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Sekta na Taasisi za kimkakati kilichofanyika kilichofanyika Machi 27, 2026 katika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara na Taasisi za kimkakati baada ya Katibu huyo kufungua kikao kazi cha kujadili matokeo ya tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Sekta na Taasisi hizo kilichofanyika kilichofanyika Machi 27, 2026 kilichofanyika kilichofanyika Machi 27, 2026 katika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma.

Washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wawezeshaji kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwenye kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu baada ya kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kilicholenga kujadili matokeo ya tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Sekta na Taasisi za kimkakati kilichofanyika katika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma.

Washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wawezeshaji kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwenye kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Nolasco Kipanda akitoa neno la utangulizi, kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Juma Mkomi kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kilicholenga  kujadili matokeo ya tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Sekta na Taasisi za kimkakati kilichofanyika  kilichofanyika Machi 27, 2026 katika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma

Washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wawezeshaji kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwenye kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa NAOT Jijini Dodoma.



 

No comments:

Post a Comment