Na Veronica Mwafisi-Mwanza
Tarehe 16 Machi, 2026
Serikali
kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imepongezwa na Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa kutekeleza Mradi
wa Zahanati katika eneo lenye changamoto ya miundombinu na kuokoa maisha ya
wakazi wa eneo hilo.
Kauli
hiyo imetolewa leo tarehe 16 Machi, 2026 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt.
Damas Ndumbaro wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua
utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya Mihama iliyopo Kata ya Kitangiri,
Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Akizungumza
kwa niaba ya kamati yake, Mhe. Dkt.
Ndumbaro amesema ujenzi wa zahanati hiyo ni msaada mkubwa kwa wakazi wa
Mihama na Kata ya Kitangiri ambao ilikuwa ni changamoto kutoka katika eneo hilo
kutafuta huduma sehemu nyingine.
“Kwa changamoto ya kufika huku, niwapongeze
TASAF kwa kutekeleza mradi huu katika eneo hili kwani itaokoa maisha ya
wananchi wa eneo hili na gharama walizokuwa wakitumia kufuata huduma za
matibabu katika eneo lingine.” Ameongeza.
Mhe.
Ndumbaro ameongeza kuwa maendeleo haya ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi ambacho kimekusudia kuwajali wananchi wake kwa kuwapa huduma
mbalimbali ikiwemo za kijamii.
Aidha,
ametoa wito kwa uongozi wa Halmashauri hiyo ya Ilemela kuhakikisha zahanati
hiyo inawekwa chini ya Halmashauri hiyo. “TASAF imetekeleza, zahanati hii ni ya
kwenu sasa, mfanye utaratibu iwe chini ya Halmashauri,” amesisitiza Mhe. Dkt.
Ndumbaro.
Naye
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema zahanati ya Mihama ni sehemu ya vielelezo vya
miradi inayotekelezwa na TASAF kwa lengo la kuwahudumia wananchi.
Mhe. Kikwete amewataka wananchi wa Mihama na Kitangiri kuitunza zahanati hiyo ili iweze kuwahudumia kama ilivyokusudiwa.
Ameongeza
kuwa, katika kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kikamilifu, katika ajira 12,000
zilizotolewa na Serikali ndani ya siku 100, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemelea
imepewa watumishi wa afya 37 na elimu 40.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa TASAF, Bw. Shadrack Mziray ameishukuru Kamati kwa
kuitembelea zahanati hiyo na kushuhudia maendeleo yaliyofanywa na Serikali
katika eneo hilo.
Akitoa neno
la shukurani kwa niaba ya wananchi wa eneo la Mihama, Bi. Mary Nyanda
ameishukuru Serikali kwa kujenga zahanati katika eneo hilo kwani walikuwa na
uhitaji mkubwa wa zahanati.
“Zahanati
hii ni mkombozi kwetu watu wa Mihama, kwa miaka 25 tumekuwa tukihangaika
kufuata huduma sehemu nyingine, tunaishukuru sana Serikali kwa kutekeleza
hili,” ameongeza Bi. Nyanda.
Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, imehitimisha ziara yake ya kikazi
ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Geita
na jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas
Ndumbaro akizungumza mara baada ya kukagua
utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya Mihama uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii (TASAF) iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya
Ilemela, Mkoani Mwanza.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani)
alipokuwa akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro kuzungumza na Watumishi wa Zahanati
ya Mihama na Wananchi wa Mihama wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua
utekelezaji wa mradi wa Zahanati hiyo uliotekelezwa na TASAF iliyopo Kata ya
Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha
Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt, Damas Ndumbaro
wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya
Mihama uliotekelezwa na TASAF iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri
ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Sehemu ya Wauguzi na
Maafisa Tabibu wa Zahanati ya Mihama wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas
Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya Mwenyekiti
huyo na Kamati yake kukagua
utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya Mihama uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii (TASAF) iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya
Ilemela, Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas
Ndumbaro na Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete
wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakikagua utekelezaji
wa mradi wa Zahanati ya Mihama uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela,
Mkoani Mwanza. Wengine ni Viongozi wa Mkoa wa Mwanza, Watendaji wa TASAF na
Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi
wa TASAF, Bw. Shadrack Mziray (kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria
iliyolenga kukagua
utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya Mihama uliotekelezwa na TASAF iliyopo Kata
ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Sehemu ya Wananchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas
Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya Mwenyekiti
huyo na Kamati yake kukagua
utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya Mihama uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii (TASAF) iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya
Ilemela, Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas
Ndumbaro akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya
Zahanati ya Mihama wakati wa ziara ya kikazi iliyolenga
kukagua
utekelezaji wa mradi wa Zahanati hiyo uliotekelezwa
na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo Kata ya
Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza. Kulia ni
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Edwin Swalle
Mwonekano wa jengo la Zahanati ya Mihami lililojengwa
na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) lililopo katika Kata ya
Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza ambapo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ilitembelea
kukagua mradi wa utekelezaji wa Zahanati hiyo.
Mkurugenzi
wa TASAF, Bw. Shadrack Mziray akitoa neno la shukrani kwa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa kufanya ziara ya kikazi kutembelea mradi
wa ujenzi wa Zahanati ya Mihama kwa lengo la kukagua
utekelezaji wa mradi wa Zahanati hiyo iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri
ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akijadili jambo na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati hiyo iliyopo Kata ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza. Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro
Bi. Mary
Nyanda akitoa shukrani kwa niaba ya Wananchi kwa Serikali kupitia TASAF kwa
kujenga zahanati ya Mihama iliyopo katika Kata ya Kitangiri, Halmashauri
ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Wanakikundi cha
Wasikivu-TASAF wakimsikiliza
Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas
Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya Mwenyekiti
huyo na Kamati yake kukagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya
Mihama uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo Kata ya
Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Mwonekano wa vifaa vya Zahanati ya Mihama iliyopo katika Kata
ya Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Sehemu ya Watendaji wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) pamoja na Maafisa wa Ulinzi na Usalama wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas
Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya Mwenyekiti
huyo na Kamati yake kukagua utekelezaji wa mradi wa Zahanati ya
Mihama uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo Kata ya
Kitangiri, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.

No comments:
Post a Comment