Saturday, March 14, 2026

MKANDARASI ATAKIWA KUKAMILISHA JENGO LA MAADILI KANDA YA ZIWA MWEZI JUNI, 2026

 

MKANDARASI ATAKIWA KUKAMILISHA JENGO LA MAADILI KANDA YA ZIWA MWEZI JUNI, 2026

Na Veronica Mwafisi-Mwanza

Tarehe 15 Machi, 2026

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imetoa malekezo ya kukamilika kwa wakati Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Ziwa ili kuweza kuwahudumia kwa ufasaha viongozi katika maeneo ya kanda hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 15 Machi, 2026 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt.  Damas Ndumbaro wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa jengo hilo lililopo eneo la Buswelu, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza. 

Akitoa maelekezo hayo kwa niaba ya kamati yake, Mhe. Dkt. Ndumbaro amesema kukamilika kwa jengo hilo kutawaondolea adha viongozi wa Kanda ya Ziwa wanaohitaji huduma katika Ofisi za Maadili ya Viongozi wa Umma.

“Jengo hili limeanza kujengwa tangu mwaka 2024 na sasa tuko mwaka 2026, Mkandarasi, kamilisha jengo hili mwezi Juni, 2026, Serikali haijawahi kudhulumu mtu, fedha zako utalipwa tu,” Mhe. Dkt. Ndumbaro ameongeza.

Aidha, ameielekeza taasisi hiyo kuboresha utaratibu wa ujazaji wa Tamko la Rasilimali na Madeni, badala ya kusubiri mpaka mwisho wa mwaka basi mfumo uwe wazi ili kurahisisha ujazaji wake na kuepuka ujazaji wa pamoja ambapo wakati mwingine mtandao umekuwa ukizidiwa.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema lengo la ujenzi wa Jengo la Maadili Kanda ya Ziwa ni kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa Viongozi wanaotumia muda mwingi kusafiri kufuata huduma hizo jijini Dodoma.

“Mhe. Mwenyekiti, tupo tayari wakati wote kupokea maelekezo ya Kamati yako kwani ukaguzi mnaoufanya unatusaidia kuboresha na kusimamia suala la maadili kwa umakini,” ameongeza

Akiwasilisha taarifa ya mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Kamishna wa Maadili, Mhe. Jaji (Stahiki) Sivangilwa Mwangesi amesema jengo hilo likikamilika litaokoa kiasi cha milioni 70 ambazo zimekuwa zikilipwa kila mwaka kwa ajili ya pango.

Kamishna Mwangesi ameahidi kuendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kutoa huduma kama ilivyokusudiwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza mara baada ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa jengo hilo lililopo Buswelu, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza mara baada ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma lililopo Buswelu, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza. Wengine ni Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt, Damas Ndumbaro wakati wa ziara ya kikazi katika Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa jengo hilo lililopo Buswelu, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.

 


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakitoka kusikiliza maelezo kuhusu Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa jengo hilo lililopo Buswelu, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.

 


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (wa pili kutoka kulia) akielekea kukagua utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo eneo la Buswelu, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete



Kamshina wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Sivangilwa Mwangesi (aliyesimama) akielezea utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa jengo hilo lililopo Buswelu, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.

Mwonekano wa jengo la Mradi wa ujenzi wa Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma lililopo Buswelu, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo kwa Msimamizi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kutoka Kampuni ya Kiure Engineering Mhandisi Sumai Mbezi mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kukagua utekelezaji wa Mradi wa jengo hilo lililopo Buswelu, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati yake mara baada ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Buswelu, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete na kushoto kwake ni Kamshina wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Sivangilwa Mwangesi.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji na Watumishi wa Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Ofisi hiyo iliyopo Buswelu, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete na kushoto kwake ni Kamshina wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Sivangilwa Mwangesi.

 

 




 

No comments:

Post a Comment