Na. Mwandishi Wetu-Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete amesema maendeleo ya
kiuchumi hayawezi kupatikana bila amani na utulivu, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha analinda na kudumisha amani hiyo.
Mhe. Kikwete ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi kwenye futari iliyoandaliwa na Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) iliyofanyika katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es salaam.
Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na mazingira ya
amani na mshikamano ambao umeifanya kuwa moja ya nchi zinazovutia
wawekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki, hivyo amewasisitiza
wananchi kutumia kipindi cha mfungo kuliombea Taifa letu amani na mshikamano
vizidi kutawala.
Mhe. Kikwete
ameongeza kuwa, katika kipindi cha mfungo, watu hufundishwa uwajibikaji na kuwa waaminifu jambo ambalo ni
muhimu na linalopaswa kuonekana si wakati wa mfungo tu bali hata katika
utekelezaji wa majukumu ya kila siku kwa ujumla ili kujenga taasisi imara zenye kuaminika.
Mhe. Kikwete amesema,
sekta ya bima na sekta ya fedha kwa ujumla
zina nafasi muhimu sana katika maendeleo ya uchumi wa Taifa kwani bima ni chombo muhimu kinachosaidia kulinda
mali, biashara na maisha ya wananchi dhidi ya hatari mbalimbali.
Amesisitiza kuwa, katika mazingira ya kisasa ya biashara na
uwekezaji, hakuna uchumi unaoweza kukua bila kuwa na mfumo imara wa bima, Serikali inahitaji taasisi imara za kifedha
zinazoweza kusaidia katika kusimamia hatari na kuhakikisha ustawi wa uchumi, wafanyabiashara wanahitaji uhakika wa kulindwa mitaji yao na wawekezaji wanahitaji mazingira salama ya
kufanya biashara zao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na wadau wa taasisi za umma, sekta binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo alipokuwa mgeni rasmi kwenye futari iliyoandaliwa na Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) iliyofanyika katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa taasisi za umma, sekta binafsi na wadau
mbalimbali wa maendeleo
alipokuwa mgeni rasmi kwenye futari iliyoandaliwa na Shirika
la Bima la Zanzibar (ZIC) iliyofanyika
katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na
taasisi za umma, sekta binafsi na wadau mbalimbali wa
maendeleo alipokuwa mgeni rasmi
kwenye futari iliyoandaliwa na Shirika la Bima la Zanzibar
(ZIC) iliyofanyika
katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es salaam.



No comments:
Post a Comment