Tuesday, March 10, 2026

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIPONGEZA OFISI YA RAIS-UTUMISHI KWA USIMAMIZI THABITI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 10 Machi, 2026.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa usimamizi thabiti wa miradi ya maendeleo nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati akiongoza kikao cha Kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.

“Kwa niaba ya Kamati yangu nitoe pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan maana ndiye mwenye ofisi hii, kwa hakika mnafanya kazi nzuri kwa kumwakilisha Mhe. Rais.” Amesema Mhe. Dkt. Ndumbaro

Vilevile, Mhe. Dkt. Ndumbaro amempongeza na kumshukuru Waziri Kikwete kwa taarifa nzuri aliyoiwasilisha kwa Kamati hiyo iliyoelezea kwa kina utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambayo itaongeza chachu ya maendeleo nchini.

Mhe. Dkt. Ndumbaro ameiahidi Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kuwa itashirikiana nayo katika usimamizi wa masuala mbalimbali ili kuleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotengewa fedha kwa mwaka 2025/2026, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema, utekelezaji wa shughuli zilizopangwa katika kipindi husika umefanyika kwa kuzingatia fedha zilizopatikana pamoja na muda wa upatikanaji wake.

Mhe. Kikwete amesema kuwa, lengo la miradi hiyo ni kuongeza tija nchini lakini pia itaongeza chachu ya utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma

Aidha, Mhe. Kikwete ameishukuru na kuiahidi Kamati hiyo kuwa Ofisi anayoisimamia itaendelea kushirikiana nao katika kuimarisha na kuboresha utendaji kazi ili kuleta tija katika kuwahudumia wadau mbalimbali kwa lengo la kujenga na kuimarisha Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongoza kikao cha Kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo jijini Dodoma leo kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.


Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais- UTUMISHI na Taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo jijini Dodoma leo kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika kikao kilichofanyika Bungeni leo jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akitazama nyaraka zake kabla ya kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika kikao kilichofanyika Bungeni leo jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wake Mhe. Regina Qwaray.


Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.

Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakijadili jambo wakati wa kikao cha Kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.


Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Mahendeka (kushoto) na Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (kulia) wakiwa kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.


Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (kulia) na Kamshina wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Sivangilwa Mwangesi (kushoto) wakiwa katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026


Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakijadili jambo wakati wa kikao cha Kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.

Sehemu ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akiongoza kikao cha Kamati yake na Watendaji wa ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026


Watendaji wa Ofisi ya Rais-IKULU na Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifafanua jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026. 


Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia taarifa ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo wakati wa kikao cha Kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.


Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli (wa kwanza kulia) pamoja na watendaji wa ofisi hiyo wakiwa kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.


Sehemu ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akiongoza kikao cha Kamati yake na Watendaji wa ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifafanua hoja wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026. 

Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akifafanua hoja iliyowasilishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.


Watendaji wa Ofisi ya Rais-IKULU na Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026. 














































 

No comments:

Post a Comment