Na. Veronica Mwafisi na Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 26 Machi, 2026.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amezielekeza Taasisi za Serikali kuanzisha Msimbo Mraba (QR CODE) utakaowezesha kutoa mrejesho wa huduma zinazotolewa na Taasisi hizo kwa wananchi.
Bw.
Mkomi ametoa maelekezo hayo leo alipokuwa akifungua kikao kazi cha wakuu wa
Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kuhusu matumizi na usimamizi wa
Mfumo wa Kielekroni (e-Mrejesho) Toleo la Pili kilichofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Bw.
Mkomi amesema ushughulikiaji wa huduma za mrejesho zinazotolewa na Serikali ni
utaratibu uliowekwa mahususi kwa lengo la kuimarisha uwajibikaji na usikivu
ndani ya Taasisi za Umma pamoja na kukuza misingi ya Utawala Bora.
Katibu
Mkuu Mkomi amewataka wasimamizi wa Rasilimaliwatu katika Taasisi hizo kuwa na
uelewa wa pamoja katika kutoa huduma na kuona namna ya kupata mrejesho kwa
jinsi inavyowaridhisha wahusika katika Utumishi wa Umma.
Vilevile,
Bw. Mkomi amewataka washiriki wa kikao kazi hicho kufuatilia kwa karibu
utekelezaji wa Mfumo wa e-Mrejesho katika taasisi zao ili waweze kutoa elimu
hiyo kwa watumishi wengine waliopo katika taasisi zao kwa lengo la kuimarisha
utendaji kazi.
Kadhalika,
Bw. Mkomi ameongeza kuwa ili kuboresha utekelezaji huo wa Mfumo wa e-Mrejesho
amewataka Maafisa Tehama kutengeneza QR CODE kwenye taasisi zote ili
kuwezesha wananchi kuutumia na kupeleka
malalamiko yao au mrejesho
kwenye taasisi husika
“Katika
wananchi 100 hautakosa wananchi 60 wenye simu za kupangusa hivyo, huduma hiyo ya
QR CODE kwa asilimia 60
itaenda mbali zaidi kwa muda mfupi,’’ amesema Bw. Mkomi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili,
Bi. Felista Shuli amesema lengo la kikao kazi hicho ni washiriki kuwezeshwa,
kupitishwa na kujadili kwa pamoja kuhusu usimamizi na utekelezaji
wa mfumo wa mrejesho ambao ni mojawapo ya mifumo iliyowekwa na Serikali kwa
lengo la kusimamia uwajibikaji katika Utumishi wa Umma.
Akitoa neno la shukrani
kwa mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mwenyekiti wa
Kikao kazi hicho ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Michael John
amemuahidi Katibu Mkuu Mkomi kuwa watazingatia maelekezo yote ambayo ameyatoa
ili waweze kuboresha utendaji kazi kwa ustawi wa Taifa.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akizungumza na Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kabla ya kufungua Kikao kazi kuhusu matumizi na Usimamizi wa Mfumo wa Kielektroni (e-Mrejesho) Toleo la pili kilichofanyika Machi 26, 2026 katika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma
Mkurugenzi
wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Bi. Felista Shuli (kushoto) akifuatilia majadiliano ya Mada
mbalimbali za kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu kuhusu matumizi na usimamizi wa Mfumo wa Kielektroni
(e-Mrejesho) Toleo la pili kilichofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu
na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa kikao hicho, Bw. Michael John.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili wa Ofisi hiyo Bi. Felister
Shuli (kulia) baada ya kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu kuhusu matumizi na usimamizi wa Mfumo wa Kielektroni
(e-Mrejesho) kilichofanyika Machi 26, 2026 katika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu
na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Bi. Janeth Mishinga akiwasilisha mada kuhusu matumizi na usimamizi wa Mfumo wa Kielektroni
(e-Mrejesho) toleo la pili katika kikao cha Wakuu wa Idara za Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu kilichofanyika Machi 26, 2026 katika Ukumbi wa
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akisalimiana na baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu baada ya kufungua Kikao kazi kuhusu matumizi na Usimamizi wa Mfumo wa Kielektroni (e-Mrejesho) Toleo la pili kilichofanyika Machi 26, 2026 katika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akisalimiana na baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu baada ya kufungua Kikao kazi kuhusu matumizi na Usimamizi wa Mfumo wa Kielektroni (e-Mrejesho) Toleo la pili kilichofanyika Machi 26, 2026 katika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akiwa
katika picha ya pamoja na Washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala
na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kuhusu kujadili matumizi
na usimamizi wa Mfumo wa Kielektroni (e-Mrejesho) kilichofanyika katika
Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi
kutoka Ofisi hiyo baada ya kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu kilichofanyika machi 26, 2026 katika Ukumbi wa
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili wa
ofisi hiyo Bi.Felista Shuli (kushoto). Kulia ni Mkurugenzi wa
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Bw. Michael John ambaye ni Mwenyekiti wa kikao kazi cha Wakuu
wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kilichofanyika Machi 26,
2026 katika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti
ya Ofisi hiyo baada ya kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu kilichofanyika machi 26, 2026 katika Ukumbi wa
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma
No comments:
Post a Comment