Na Veronica Mwafisi-Mwanza
Tarehe 15 Machi, 2026
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeelekeza nyaraka
kuhifadhiwa katika mfumo wa kidijiti ili kuwezesha kizazi cha sasa kujua
historia ya nchi na kulinda amani kwa maendeleo ya taifa.
Kauli
hiyo imetolewa leo tarehe 15 Machi, 2026 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt.
Damas Ndumbaro wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua
utekelezaji wa Mradi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka Kanda ya Ziwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Akitoa
maelekezo hayo kwa niaba ya kamati yake, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kizazi
cha sasa kutokujua historia ya nchi yao kumesababisha kutoona umuhimu wa
kuitunza amani ya nchi.
“Kuna
umuhimu sasa yale mambo ya kihistoria ambayo siyo nyeti tuyachambue ili
yawafikie vijana, tujivunie utaifa wetu, tusisubiri watoto wetu wafunzwe na
ulimwengu, tuwawekee nyaraka zitakazosaidia kujua historia ya nchi yao kwenye
mfumo wa kidijiti.” Mhe. Dkt. Ndumbaro amesisitiza.
Aidha, kamati
hiyo imempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Bw.
Firimin Msiangi pamoja na wasaidizi wake kwa kazi nzuri wanayoifanya ya
utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka kwa ajili ya vizazi vijavyo.
“Kazi
nzuri sana imefanyika, tumeona, changamoto ya bajeti mliyonayo tunamuelekeza
Waziri ifanyiwe kazi kwa kutoa kipaumbele kwenye kuziweka nyaraka katika mfumo
wa kidijiti na masilahi ya watumishi wa Idara hii nyeti,” ameongeza Mhe. Dkt.
Ndumbaro.
Kwa
upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ametoa wito kwa wajumbe wa kamati hiyo kuitumia
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kujifunza historia ya nchi na kuona
nyaraka ambazo zitawasaidia katika shughuli zao hasa kwa wanaohitaji kuandika
vitabu.
“Kituo
hiki kina utajiri wa kumbukumbu na nyaraka, kwa wanaotaka kujifunza historia ya
nchi yetu na kuandika vitabu, mtumie kituo hiki, tumeona nchi hii ilivyo na
historia ndefu, mtapata taarifa nyingi.” Mhe. Kikwete amesisitiza.
Vile vile
Mhe. Kikwete amewasisitiza wajumbe hao wa kamati kujifunza kuweka kumbukumbu
zao na kuwarithisha vizazi vijavyo. “Wenzetu huko nyuma walikuwa wanaandika na
ndio maana tumeweza kuona historia nzuri ya nchi yetu, basi sasa nasi tujifunze
kufanya hivyo kwa vizazi vyetu vijavyo,” Mhe. Kikwete ameongeza.
Akiwasilisha
taarifa ya Mradi wa Kituo hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na
Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi alisema lengo la uanzishwaji wa kituo hicho ni
kusogeza huduma ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka za taasisi za serikali kwa
Kanda ya Ziwa ili kulinda urithi wa kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria,
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza
mara baada ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka
Kanda ya Ziwa, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro kuzungumza na Watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka wakati wa ziara ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka Kanda ya Ziwa, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa
maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt, Damas Ndumbaro wakati
wa ziara ya kamati hiyo katika Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa
iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kituo cha
Kumbukumbu na Nyaraka Kanda ya Ziwa, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela,
Mkoani Mwanza
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala, Katiba na Sheria wakimsikiliza Afisa
Kumbukumbu, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka, Bi. Maryam Ayoub (wa kwanza kushoto)
alipokuwa akitoa maelezo kuhusu Vita vya Kagera kwa Wajumbe hao wakati wa ziara
ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa
Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka Kanda ya Ziwa, Halmashauri ya Wilaya ya
Ilemela, Mkoani Mwanza
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani)
alipokuwa akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) kuzungumza na
Watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka wakati Kamati hiyo ilipotembelea na
kukagua
utekelezaji wa Mradi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka Kanda ya Ziwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akivalishwa skafu
mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka
wakati wa ziara ya kikazi na Kamati yake iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa kituo hicho kilichopo Kanda ya
Ziwa, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (wa kwanza kushoto) akifuatilia jambo pamoja na Wajumbe wa Kamati yake walipokuwa wakipatiwa maelezo mbalimbali ndani ya ghala la kuhifadhia nyaraka wakati wa ziara ya kikazi katika Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa kituo hicho kilichopo Kanda ya Ziwa, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala, Katiba na Sheria wakimsikiliza Mkurugenzi
Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Kituo
cha Kumbukumbu na Nyaraka wakati Kamati hiyo
ilipotembelea na kukagua utekelezaji wa Mradi wa hicho
kilichopo Kanda ya Ziwa, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka Kanda ya Ziwa, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza. Wengine ni Watendaji wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka.
Mkurugenzi
Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala, Katiba na Sheria wakati kamati hiyo ilipokuwa ikikagua utekelezaji
wa Mradi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka Kanda ya Ziwa, Halmashauri
ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI
na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) akizungunmza jambo na
Mkurugenzi Mkuu wa Idara
ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi (kulia) walipokuwa
wakiisubiri Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kikazi ya
Kamati hiyo iliyolenga kukagua
utekelezaji wa Mradi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka Kanda ya Ziwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza. Wa kwanza kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyrus Kapinga (kulia) akiteta jambo
na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka
za Taifa, Bw. Firimin Msiangi (kushoto) walipokuwa wakiisubiri Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria
wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa
Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka Kanda ya Ziwa, Halmashauri ya Wilaya ya
Ilemela, Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na
Watendaji wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka mara baada ya kuwasili katika Kituo
cha Kumbukumbu na Nyaraka wakati wa ziara ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa kituo hicho kilichopo Kanda ya
Ziwa, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.



No comments:
Post a Comment