Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe: 9 Machi, 2026.
Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amewataka watumishi wa Ofisi hiyo kutumia na
kuzingatia elimu waliyopewa ya Usalama Mahali Pa Kazi kuepukana na changamoto
zinazoweza kujitokeza kutokana dharura mbalimbali ili kuondoa hofu ya kimwili
na kiakili wanapokuwa wanawajibika katika maeneo yao ya kazi.
“Tumepatiwa
elimu kuhusu Usalama Mahali pa Kazi, nitoe wito kwenu kuzingatia elimu hii kwa
manufaa yetu sote ili kuondokana na hofu na kujenga uwajibikaji ulio bora
tutakapokuwa tunatekeleza majukumu yetu katika maeneo ya kazi.” Bw. Daudi
alisema.
Aidha,
Bw. Daudi amewasisitiza watumishi hao kuzingatia suala la usafi wa mazingira wawapo
katika maeneo yao ya kazi jambo ambalo litaongeza ufanisi katika utendajikazi kwani
afya bora ni mtaji wa uwajibikaji utakaomwezesha mtumishi wa umma kutoa huduma
bora itakayoongeza imani ya Wananchi kwa Serikali yao.
Vilevile,
Bw. Daudi amempongeza Mkaguzi wa Mazingira ya Kazi kutoka Wakala wa Usalama na
Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bw. Thadei Mwasamila kwa kutoa elimu hiyo kwa
ufasaha kwani itasaidia kuongeza chachu ya utendajikazi kwa Waajiri na Watumishi.
Kwa
upande wake, Bw. Mwasamila ametoa rai kwa waajiri na watumishi wa umma kuhakikisha
wanazuia ajali mahali pa kazi ili kuwa na amani na kuondokana na hofu
wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.
Mkaguzi wa Mazingira ya Kazi
kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bw. Thadei Mwasamila
akiwasilisha mada ya Usalama Mahali Pa Kazi kwa Watumishi wa Ofisi ya Rais
-UTUMISHI wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika Machi 9, 2026
katika Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma
Sehemu ya Wakurugenzi na
Watumishi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na mwezeshaji juu ya Usalama Mahali Pa
Kazi yaliyofanyika Mtumba Jijini Dodoma
Sehemu ya Wakurugenzi na
Watumishi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na mwezeshaji juu ya Usalama Mahali Pa
Kazi yaliyofanyika Mtumba Jijini Dodoma
No comments:
Post a Comment