Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 23 Machi, 2026
Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi amewataka watumishi wa Ofisi yake kuzingatia
sheria na kanuni za maadili ya
utumishi wa umma na kutumia ujuzi wa kitaaluma walionao ili kutoa huduma
bora kwa umma.
Bw. Mkomi ameyasema hayo
wakati akihitimisha mafunzo ya kila wiki ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yaliyofanyika katika
eneo maalumu la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma.
“Naomba nitoe rai kwenu kuwa
kila mtumishi wa Umma kwa nafasi yake ahakikishe anatekeleza majukumu yake kwa uwazi,
uaminifu, weledi na ufanisi ili kuepusha malalamiko ya wananchi kwa Serikali” alisema
Bw. Mkomi.
Vile vile Bw. Mkomi
amezishukuru na kuzipongeza Kurugenzi husika zilizoandaa mada pamoja na watoa
Mada kwa uwasilishaji wao mzuri ambao umetoa uelewa utakaoboresha utendaji kazi
wa watumishi wa umma.
Awali, Mchambuzi Kazi
Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji Taasisi Bw. MacDonald Kiwis wakati
akiwasilisha mada ya Uandishi wa Nyaraka za Serikali alisema kuwa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Taasisi zote za Umma kwa jumla hazina budi kufuata miongozo ya
uandishi wa nyaraka za Serikali ili kuwa na viwango vinavyofanana.
Mchambuzi Kazi Mwandamizi
kutoka Idara ya Uendelezaji Taasisi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Bw. MacDonald Kiwis akitoa ufafanuzi kuhusu Miongozo ya
Uandishi wa Nyaraka za Serikali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi
wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaliyofanyika machi 23, 2026 jijini Dodoma.
Sehemu ya watumishi wa Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati alipokuwa
akihitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Mtumba Jijini Dodoma.

No comments:
Post a Comment