Na. Lusungu Helela-Arusha
Tarehe 10 Julai, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema rushwa Barani Afrika ni tatizo linalohitaji njia ya pamoja ya kupambana nalo kwani utoaji na upokeaji rushwa unabadilika kulingana na msukumo wa maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja maisha ya watu kadiri yanavyobadilika.
Imeelezwa kuwa ni muda muafaka sasa kwa nchi za Afrika kuwa na sheria zinazofanana katika kushughulikia tatizo hilo, hali itakayopelekea kutokomeza kabisa tatizo la rushwa.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa, ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha, Mhe. Simbachwene amesema mbinu za kupambana na rushwa ni lazima kubadilika kulingana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Amesema kongamano hilo ikiwezekana litoke na maazimio ya pamoja yatakayopelekea nchi zote za Afrika kuwa na sheria zinazofanana ili watuhumiwa wa rushwa wa nchi hizo wajue kabisa kuwa watawajibishwa kupitia sheria hizo.
Amesema kuwa tatizo la rushwa Barani Afrika ni kubwa na linahitaji sauti ya pamoja huku akitolea mfano wa rushwa kwenye suala la utoaji wa elimu na kusema kuwa kama hatua za pamoja hazitachukuliwa kutapelekea kuwa na vijana wahitimu ambao ni zao la rushwa.
Kufuatia hatua hiyo amezihimiza nchi za Afrika kutumia Kongamano hilo kujadili namna bora ya kutumia sayansi na teknolojia katika utoaji huduma utakaowezesha kuzuia watu kukutana ana kwa ana huku akisisitiza mifumo hiyo iwekwe ili kudhibiti rushwa katika sekta mbalimbali.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) CP. Salum Hamduni amesema Kongamano hilo, mbali ya kuwakutanisha Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika pia limewakutanisha Wadau wa kupambana na rushwa wa ndani na nje ya nchi, hivyo Kongamano hilo ni darasa huru la kujifunza na kupata uzoefu wa kupambana na rushwa kwa nchi moja moja na Afrika kwa ujumla ili kuhakikisha kuwa rushwa inatokomezwa kabisa.
Ameongeza
kuwa Kongamano hilo pamoja na kujadili mada mbalimbali za kupambana na rushwa Barani
Afrika pia watajadili mbinu mbalimbali za kupambana na tatizo hilo kidigitali
ikizingatiwa kuwa utoaji wa rushwa kwa sasa unafanyika kidigitali.
Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufikia tamati kesho Julai 11, 2023 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifungua Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa
ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani
Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo
yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) CP Salum Hamduni akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kufungua Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano
la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano hilo ikiwa
ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika
ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo

No comments:
Post a Comment