Na. Veronica Mwafisi-Kibaha
Tarehe 10 Julai, 2023
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza nia yake ya dhati katika kuwafikia Watanzania wenye mahitaji kupitia mradi wa TASAF ili kuwanusuru wananchi walio na hali duni ya maisha.
Mhe.
Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Mtaa wa Miwaleni, Tarafa ya Kongowe, Wilaya ya Kibaha
wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji
wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Mhe.
Kikwete amesema kuwa, katika utekelezaji wa majukumu ya Rais Mhe. Dkt. Samia
ndani ya miaka miwili ya uongozi wake zaidi ya Shilingi bilioni hamsini na moja
zimeweza kutumika ili kuwasaidia wananchi wenye hali duni ambao wanakidhi
kunufaika na mradi wa TASAF.
Mhe.
Kikwete amewataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kumuunga
mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyedhihirisha
nia yake ya dhati kwa vitendo katika kuwainua kimaisha Watanzania wenye hali
duni kupitia mradi wa TASAF.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon amewapongeza walengwa
wa TASAF, wanaofanya biashara kupitia mikopo mbalimbali wanayoipata kutokana na
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Naye, mlengwa
wa TASAF, Bi. Mariam Pazzi amesema kwa niaba ya walengwa wenzake wa TASAF
wanamshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia kwa kuwawezesha kupata mikopo mbalimbali
ambayo imewawezesha kufanya biashara kupitia vikundi mbalimbali hivyo kuwawezesha
kuinuka kimaisha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete yupo katika ziara ya kikazi ya wiki moja katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao pamoja na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Mtaa
wa Miwaleni, Tarafa ya Kongowe, Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu
Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri
ya Mji Kibaha.
Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon akitoa neno la
utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete kuzungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Mtaa wa
Miwaleni, Tarafa ya Kongowe, Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya kikazi ya
Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika
Halmashauri ya Mji Kibaha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akimtambulisha
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF), Bw. Henry Mbago (kushoto) kwa wananchi na walengwa wa
TASAF wa Mtaa wa Miwaleni, Tarafa ya Kongowe, Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara
ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya
TASAF katika Halmashauri ya Mji Kibaha.
Mlengwa wa TASAF, Bi. Mariam Pazzi akitoa shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
kwa kufanya ziara katika Mtaa wa
Miwaleni, Tarafa ya Kongowe, Wilaya ya Kibaha kwa lengo la kukagua utekelezaji
wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Kibaha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitazama baadhi ya
bidhaa za walengwa wa TASAF zinazouzwa katika Mtaa wa Miwaleni, Tarafa ya
Kongowe, Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Kibaha.
No comments:
Post a Comment