Wednesday, July 5, 2023

WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA KIKAO KAZI NA WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA MAADILI NA KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO JIPYA LA OFISI HIYO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma (hawapo pichani) jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.


Sehemu ya watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watumishi hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na watumishi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watumishi hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.


Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi (Aliyesimama) akielezea utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Meza kuu) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati) akizungumza jambo na Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete (Wa kwanza kushoto) mara baada ya kukagua jengo jipya la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati) mara baada ya kukagua jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi.


Mwonekano wa jengo jipya la Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambalo ujenzi wake unaendelea jijini Dodoma.

 

 


 

No comments:

Post a Comment