Na. Veronica Mwafisi-Kibaha
Tarehe 11 Julai, 2023
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema moja kati ya mbinu ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza kwa wananchi wote ni kushiriki katika kubuni mbinu mbalimbali zitakazowawezesha wananchi kujimudu na kuendesha maisha yao pasipokuwa na changamoto yoyote.
Mhe. Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata ya Janga, Mtaa wa Mwembebaraza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Mhe.
Kikwete amesema kuwa, Rais Dkt. Samia amekuwa akitoa fedha nyingi ili ziweze
kutumika kupitia mbinu na ubunifu mkubwa wenye ubora ili kuweza kuwainua
wananchi kiuchumi.
Mhe.
Kikwete ametoa pongezi kwa wananchi na watendaji wakiwemo viongozi mbalimbali
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa kuhakikisha utekelezaji wa majukumu
mbalimbali ya miradi ya TASAF inatekelezeka kupitia kilimo cha kisasa.
Mhe.
Kikwete amesema tangu aanze ziara za kikazi katika baadhi ya mikoa amekuwa
akikutana na shuhuda na bunifu wa vitu mbalimbali hivyo ni dhahiri kuwa
wananchi na walengwa wa TASAF wamekuwa wakifaidika kupitia bunifu za vitu
mbalimbali.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon amesema wananchi wa
taifa la Tanzania ni watu wenye ukarimu hivyo ni vizuri wakaendelea kushirikiana
kwa kuwainua walio chini na kupitia mradi wa TASAF jambo ambalo linatekelezeka
kwa asilimia kubwa.
Naye,
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Bi. Sijaona Muhunzi amesema
katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wanatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo
ajira za muda, mradi wa kuweka akiba na kukuza.
Katika hatua nyingine, Mhe. Naibu waziri Kikwete amefanya kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Kibaha ambapo amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kujiwekea malengo ya utendaji kazi ili kuboresha kazi zao kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete anaendelea na ziara ya kikazi ya wiki moja katika Mkoa wa Pwani kwa
lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi hao pamoja na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza
na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata
ya Janga, Mtaa wa Mwembebaraza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakati wa
ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi
ya TASAF.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akitazama miti ya mbogamboga katika shamba darasa la kilimo
cha kisasa kinachotekelezwa na kikundi cha walengwa wa TASAF katika Halmashauri
ya Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Mwonekano wa kilimo cha kisasa cha nyanya kinachotekelezwa
na kikundi cha walengwa wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
Sehemu ya watumishi wa Mkoa wa Pwani
katika Halmashauri ya Wilaya Kibaha wakimsikiliza Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya
kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua
changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon akitoa neno la
utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha
wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji
na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Mkoa wa Pwani,
Mhe. Michael Mwakamo akitoa salamu za wananchi na watumishi wa jimbo lake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa ziara ya
kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua
changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akipokea salamu kutoka kwa Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili katika ofisi za Halmashauri ya
Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya Kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na
kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
No comments:
Post a Comment