Na. Lusungu Helela-Kibakwe
Tarehe 18 Julai, 2023
Wananchi wa
Kata ya Malolo iliyopo Jimbo la Kibakwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
wamepaza sauti zao kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakimuomba asaidie kubadili
mchakato wa kuwapata walengwa halisi wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) huku wakisisitiza kuwa
utaratibu unaotumika kwa sasa umegubikwa na sintofahamu.
Aidha, Wananchi
hao wamewataka walengwa wa Mpango huo ambao tayari wameimarika kiuchumi kuwa na
utu kwa kujiondoa na kuwapisha wengine wanaostahili kuingizwa kwenye Mpango.
Hayo yamesemwa
na Wananchi mbalimbali kwa nyakati tofauti kupitia mikutano ya hadhara ya
Waziri huyo anayoendelea kuifanya katika Vijiji vya Jimbo la Kibakwe ikiwa ni muendelezo
wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo wananchi hao wameomba
ubainishaji huo wa walengwa ufanyike kwa uwazi ikiwezekano kupitia mikutano ya
hadhara ili waweze kuwapata walengwa halisi.
Wamefafanua
kuwa licha ya TASAF kuwashirikisha viongozi wa vijiji husika katika kuwabaini
Walenga halisi lakini bado hawaridhishwi na jinsi mchakato unavyoendeshwa kwani
kuwekuwa na usiri wa hali ya juu.
Wamesema kuwa
mchakato huo katika ngazi za vijiji haufanyiki vizuri hivyo kupelekea wale
ambao sio maskini halisi kuwa wanufaika ilhali wale maskini halisi wakiendelea
kutaabika.
Malalamiko
hayo ya wananchi yalitokana na maswali ya Mhe. Simbachawene ya kutaka
kuwatambua walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kata hiyo ya
Malolo na namna walivyopatikana ili kujiridhisha na minongóno aliyoisikia juu
ya upatikanaji wa walengwa hao.
Akijibu
malalamiko hayo, Waziri Simbachawene amesema tayari ameshatoa maelekezo kwa
Menejimenti ya TASAF Makao Makuu kuangalia namna bora ya kuwapata walengwa
halisi wa Mpango.
Ameongeza
kuwa TASAF msingi wake ni mpango shirikishi wa kuondoa umasikini uliokithiri
kwa wananchi, hivyo ni lazima kutafuta njia sahihi ili kutimiza azma ya kuanzishwa kwake.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nzugilo wakati wa mkutano wa
hadhara na wananchi hao katika Kijiji hicho, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya
Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma uliolenga kuwasikiliza wananchi wa kijiji hicho
kuhusiana na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii (TASAF) na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi.
Sehemu ya
wananchi wa Kijiji cha Nzugilo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa
akizungumza nao wakati ziara yake ya kikazi katika kijiji hicho, Jimbo la
Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma uliolenga kuwasikiliza
wananchi wa kijiji hicho kuhusiana na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na kuelezea utekelezaji
wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mpwapwa ambaye pia ni Diwani wa Mpwapwa Mjini, Mhe. George Fuime akizungumza
kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Nzugilo wakati wa mkutano wa
hadhara na wananchi wa kijiji hicho, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya
Mpwapwa mkoani Dodoma uliolenga kuwasikiliza wananchi wa kijiji hicho kuhusiana
na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) na kuelezea utekelezaji
wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene akiwa na wananchi wa Kijiji cha Nzugilo ambao wanakijiji wenzao
waliwabaini kuwa wanastahili kuingizwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) lakini wameachwa.
No comments:
Post a Comment