Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ameridhishwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kufikisha asilimia 88 ya ujenzi wa jengo la ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Akitoa pongezi hizo leo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Serikali zinazoendelea kujengwa katika Mji huo wa Serikali, Waziri Mkuu Majaliwa amesema ujenzi wa jengo hilo la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, umefikia hatua nzuri huku akisisitiza kuwa ifikapo mwezi wa 10, 2023 jengo hilo liwe limekamilika ikiwemo mindombinu ya maji na umeme.
"Nataka ifikapo mwezi Novemba na Disemba mwaka huu, muwe mmekamilisha hatua ya kununua vifaa vya ofisi, wakati mnaendelea kukamilisha ujenzi, anzeni kutangaza zabuni kwa ajili ya kupata vifaa hivyo ili ifikapo Januari 1, 2024 Watumishi wote wawe kwenye jengo moja" amesisitiza Majaliwa.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa amewasisitiza Viongozi na Watendaji wa Ofisi hiyo kuhakikisha wanatembelea katika jengo hilo mara kwa mara kwa ajili ya kukagua ili kujua kila hatua inayoendelea kwa lengo la kukamilisha kwa wakati ujenzi.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuiwezesha Ofisi hiyo
kwa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo hilo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza mara baada ya kuwasili
katika jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
ambalo limefikia asilimia 88 ya ujenzi wake katika Mji wa Serikali Mtumba
Jijini Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya viongozi mara baada ya kuwasili katika jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambalo limefikia asilimia 88 ya ujenzi wake katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
wakati akimuelezea hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora ilipofikia.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwan Kikwete akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Daudi Kondoro wakati wakimsubiri Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kukagua jengo hilo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza
na Naibu Katibu Mkuu wake Bw. Xavier Daudi wakati wakimsubiri Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kukagua
jengo la Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa
ameongoza na Naibu Waziri wake Mhe.Ridhiwan
Kikwete wakati wakikagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambalo limefikia asilimia 88 ya ujenzi
wake katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Muonekano
wa jengo la Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambalo limefikia
asilimia 88 ya ujenzi wake katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma
No comments:
Post a Comment