Na.
Veronica Mwafisi-Kibaha
Tarehe 10
Julai, 2023
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi wa umma kuleta tija katika utendaji kazi wao ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 22 Aprili, 2021 kwa mara ya kwanza ambapo alielekeza kuwa, anataka utumishi wa umma wenye tija kwa kila mtumishi ili kutoa huduma bora kwa mendeleo kwa Taifa.
Mhe. Kikwete amesema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Mkoani Pwani akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua kero na changamoto zinazowakabili watumishi wa umma mkoani humo.
“Rais Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan alieleza wazi kuwa halmashauri zake, watendaji na
watumishi wote ni lazima wawe na tija katika utekelezaji wa majukumu yao ili
kuleta maendeleo nchini,” amesema Mhe. Kikwete.
Vile vile,
Mhe. Kikwete amewataka watumishi hao kubadilika ili kuendana na matakwa ya
Serikali ya Awamu ya Sita ikiwemo uaminifu katika utekelezaji wa miradi
mbambali ya maendeleo nchini na kwa kuzingatia ubora.
Aidha, Mhe.
Kikwete amesema kuwa, mafanikio ya taasisi au taifa lolote yanategemea aina ya
watumishi wanaoitumikia Serikali yao wakati wa utekelezaji wa majukumu ambapo
wakitekeleza kwa weledi na ufanisi mkubwa yataleta chachu kwa maendeleo ya
nchi.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi wa Mji Kibaha, Mhandisi
Mshamu Munde amemshukuru Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa
kufanya ziara katika mkoa huo na kuahidi kuwa yeye pamoja na watumishi wenzake
watatekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwani kwa kutokufanya hivyo itakuwa ni
utovu wa nidhamu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameanza
ziara ya kikazi katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa
watumishi wa umma, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma pamoja
na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF katika mkoa huo.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akizungumza na watumishi wa Mkoa wa Pwani na Halmashauri ya
Mji wa Kibaha wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo iliyolenga kuhimiza
uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Sehemu
ya watumishi wa Mkoa wa Pwani na Halmashauri ya Mji wa
Kibaha wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga
kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Mkuu wa
Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon akitoa utambulisho wa viongozi na
watendaji wa Halmashauri ya
Mji Kibaha kabla ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuzungumza nao wakati wa ziara ya
kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua
changamoto zinazowakabili katika halmashauri hiyo.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa
Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge (kulia)
wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri Kikwete iliyolenga kuhimiza
uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili katika halmashauri hiyo.
Katibu
Tawala, Mkoa wa Pwani, Bw. Rashid Mchata akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya
Mkoa wa Pwani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri
huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi wa mkoa huo.
Mkurugenzi
wa Mji Kibaha, Mhandisi Mshamu Munde akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuhitimisha kikao kazi na watumishi wa Mkoa wa Pwani na
Halmashauri ya Mji Kibaha wakati wa ziara ya kikazi
ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto
zinazowakabili.
Mtumishi
wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Bw. Issa Hasani (Aliyesimama) akiwasilisha hoja
kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo Mkoa
wa Pwani iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi hao.
No comments:
Post a Comment