Na. Veronica E. Mwafisi-Iringa
Tarehe 27 Oktoba, 2022
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi ameutaka uongozi wa Manispaa ya Iringa kuzingatia mahitaji
na maslahi ya watumishi ili kuwajengea ari na morali ya utendaji kazi katika
kuwahudumia wananchi.
Mhe. Ndejembi ametoa wito huo
kwa viongozi wa Manispaa ya Iringa, wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa
hiyo akiwa katika ziara ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamozo
zinazowakabili watumishi hao.
"Mimi naomba sana viongozi mbadilike katika
suala zima la kusimamia rasilimaliwatu, tuzingatie maslahi na mahitaji ya watumishi
wetu ili kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii, weledi na morali ya hali ya juu," Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka
wakuu wa idara katika Manispaa ya Iringa kuwa na utaratibu wa vikao vya mara
kwa mara na watumishi wanaowasimamia ili kusikiliza kero zao na kuzitatua kwa
wakati.
“Si jukumu la Mkurugenzi au
Afisa Utumishi pekee kuzungumza na watumishi, wakuu wa idara mnawajibu wa kuwa
na vikao vya kuzisikiliza kero na changamoto zinazowakabili watumishi
mnaowaongoza ili kuzitatua," Mhe. Ndejembi amehimiza.
Kuhusiana na wingi wa malalamiko
kutoka kwa watumishi, Mhe. Ndejembi amesema, uongozi wa Manispaa ya Iringa unapaswa
kufanya tathmini ya hali ya utendaji kazi kwani idadi kubwa ya watumishi
imewasilisha malalamiko.
Kwa upande wake, Mkuu wa
Wilaya ya Iringa, Bw. Mohammed Moyo amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kutenga muda
wa kusikiliza kero na malalamiko ya watumishi katika wilaya yake ikiwa ni
pamoja na kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika
halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi hao wa umma.
Watumishi
wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara
yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi hao wa umma.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw.
Mohammed Moyo akitoa neno la utangulizi kabla ya
kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa yake, wakati wa
ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua
changamoto zinazowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiteta
jambo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw.
Mohammed Moyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya
Naibu Waziri huyo katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na
kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao wa umma.
Mtumishi wa Iringa Manispaa, Bi.
Jamila Mwindi, akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji
na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi
akisikiliza hoja iliyokuwa ikiwasilishwa na mtumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakati wa ziara yake
ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo.
Katibu wa Naibu
Waziri, Bw. Philemon Mmbaga (Wakwanza kulia) akichukua taarifa za mtumishi
aliyewasilisha changamoto yake wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi aliyoifanya
katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment