Na. Veronica E. Mwafisi-Dar
es Salaam
Tarehe 19 Oktoba, 2022
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema mafunzo ya kuwajengea uwezo kiutendaji viongozi katika
Utumishi wa Umma na sekta binafsi yanayotolewa na Taasisi ya UONGOZI, yamelenga
kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita za kuimarisha Utawala Bora
nchini.
Mhe. Ndejembi amesema hayo jijini Dar es Salaam akiwa katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, wakati akizindua Awamu ya
Tatu ya Programu ya Mafunzo kwa Viongozi yanayotolewa na Taasisi ya UONGOZI.
Mhe. Ndejembi amesema, program zote za mafunzo
zinazotolewa kwa viongozi kupitia Taasisi ya UONGOZI zimelenga kuimarisha uwezo
na kuwaongezea ufanisi kiutendaji kwenye maeneo yao ya kazi.
“Programu hizi za mafunzo kwa viongozi zinazoandaliwa
na Taasisi ya UONGOZI zinalenga kuimarisha uwezo wa viongozi katika kufanya
maamuzi ya kimkakati, kuongoza rasilimaliwatu na kujenga sifa binafsi za
kiongozi,” Mhe. Ndejembi amesema.
Ameongeza kuwa, mafunzo hayo yanayotolewa kwa
viongozi kupitia Taasisi ya UONGOZI ni muhimu katika kuimarisha utawala bora
utakaokuwa ni chachu ya kuleta maendeleo endelevu nchini.
Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka washiriki wa
mafunzo hayo, kuyazingatia mafunzo kikamilifu ili kupata elimu na ujuzi utakaowaongezea
ufanisi kiutendaji na kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao ya kazi pindi
watakapohitimu.
Sanjali na hilo, Mhe. Ndejembi amesema mafunzo
hayo yameandaliwa katika viwango vya kimataifa ili kuwajenga viongozi kifikra
na kimtazamo, kwa kuwapatia uelewa mpana katika masuala ya uongozi na hatimaye
kuwa na mchango katika maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake, mmoja wa washiriki wa mafunzo
hayo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Afya Plus, Dkt. Pastory Sekule amesema,
baada ya kuhitimu mafunzo hayo anatarajia kupata uzoefu mkubwa zaidi
utakaomuwezesha kusimamia rasilimali pamoja na kusimamia mabadiliko kwa kuwaongoza
watumishi alionao katika eneo lake la kazi.
Jumla ya washiriki 68 kutoka katika taasisi za umma na sekta binafsi wanashiriki mafunzo hayo ya Awamu ya Tatu ya Program ya Mafunzo kwa Viongozi yanayotolewa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Serikali ya Finland pamoja na Umoja wa Mataifa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizindua Awamu ya Tatu ya Programu ya Mafunzo kwa Viongozi yanayoratibiwa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Serikali ya Finland na Umoja wa Mataifa.
Sehemu ya
washiriki wa Awamu ya Tatu ya Programu ya Mafunzo kwa Viongozi
yanayoratibiwa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Serikali ya
Finland na Umoja wa Mataifa wakimsikiliza Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi wakati akizindua mafunzo hayo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji
Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo akitoa neno la utangulizi kabla ya
kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi kuzindua Awamu ya Tatu ya Programu ya Mafunzo kwa Viongozi,
yanayoratibiwa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Serikali ya
Finland pamoja na Umoja wa Mataifa.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi akizungumza jambo na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo kabla ya
Naibu Waziri Ndejembi huyo kuzindua Awamu ya Tatu ya Programu ya Mafunzo
kwa Viongozi ambayo yanayoratibiwa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana
na Serikali ya Finland pampoja na Umoja wa Mataifa.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi (katikati) akifafanua jambo alipotembelea Maktaba ya Taasisi ya UONGOZI jijini
Dar es Salaam, kabla ya kuzindua Awamu ya Tatu ya Programu ya Mafunzo kwa
Viongozi. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu
wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Awamu ya Tatu ya Programu
ya Mafunzo kwa Viongozi, yanayoratibiwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana
na Serikali ya Finland na Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment