Na. Veronica Mwafisi - Moshi
Tarehe 14 Oktoba, 2022
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama amesema Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za
Wanyonge (MKURABITA) imekuwa chachu ya ongezeko la ukusanyaji wa mapato kupitia
vituo jumuishi vya urasimishaji na uendelezaji wa biashara ambavyo imevianzisha
katika maeneo mbalimbali nchini.
Mhe.
Jenista ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
kabla ya kuzindua Kituo Jumuishi
cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara katika Manispaa hiyo akiwa kwenye ziara
yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za MKURABITA mkoani
Kilimanjaro.
Mhe.
Jenista amesema ongezeko la ukusanyaji wa mapato kupitia vituo hivyo jumuishi
linajidhihirisha wazi kwenye Kituo Jumuishi cha
Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kilichop Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
baada ya makusanyo ya robo mwaka kuongezeka kwa shilingi 71,336,000.
“Kupitia kituo hiki jumuishi cha Manispaa ya Moshi,
Serikali imeboresha ukusanyaji wa mapato yanayotokana na ada za leseni za
biashara kwani wastani wa makusanyo ya ada hiyo kabla ya kituo hiki kuanzishwa ilikuwa
shilingi140,624,000 kwa robo mwaka lakini baada ya uwepo wa kituo hicho wastani
wa makusanyo umeongezeka na kufikia shilingi 212,000,000 ambalo ni ongezeko la
shilingi 71,376,000.
Mhe. Jenista ameipongeza
Halmashauri ya Manipaa ya Moshi kwa ongezeko hilo la ukusanyaji wa mapato
kupitia kituo hicho jumuishi kwani imeitikia wito wa Serikali wa kubuni vyanzo
mbalimbali vya ukusanyaji mapato kwa maendeleo ya taifa.
Aidha, Mhe. Jenista
ameongeza kuwa, urasimishaji umeongeza wigo wa walipa kodi kwa kuingiza
biashara ndogondogo za waendesha bodaboda na bajaji zilizorasimishwa katika
mfumo rasmi wa walipa kodi nchini.
Akielezea
faida ya uanzishwaji wa Vituo Jumuishi vya Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara,
Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania
(MKURABITA), CPA. Dkt. Seraphia
Mgembe amesema kupitia kituo jumuishi cha Manispaa ya Moshi, Serikali
imefanikiwa kusajili walipa kodi ambao hapo awali walikuwa wakiogopa kusajiliwa
kwa kutokuona umuhimu wake.
Amesema
zamani kodi ilikuwa haitamkwi hadharani lakini sasa hivi inatamkwa kwani kila
mmoja amepata ufahamu wa kuchangia pato la taifa kwa maendeleo.
“Baada
ya kuwasajili kwenye kwenye mfumo, wanatambua umuhimu wa kulipa kodi na sasa
wanaendelea kulipa, kutoa ada za leseni na wanafanya biashara zao kwa
kujiamini,” CPA Dkt. Seraphia
ameongeza.
Mhe. Jenista amefanya ziara ya
kikazi ya siku moja mkoani Kilimanjaro yenye lengo la kukagua utekelezaji wa
shughuli za MKURABITA na kuzungumza na watumishi wa mkoa huo ili kuhimiza
uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifurahi
pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Abasi Kayanda mara baada ya Waziri
Jenista kuzindua rasmi kituo Jumuishi
cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kilichopo Manispaa ya Moshi mkoani
Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa
shughuli za MKURABITA mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akijiandaa
kukata utepe ili kuzindua rasmi kituo Jumuishi
cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kilichopo Manispaa ya Moshi mkoani
Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa
shughuli za MKURABITA mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza
na baadhi ya wafanyabiashara wa Manispaa ya Moshi kabla ya kuzindua kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara
kilichopo Manispaa ya Moshi wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua
utekelezaji wa shughuli za MKURABITA mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza
na baadhi ya wafanyabiashara wa Manispaa ya Moshi kabla ya kuzindua kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara
kilichopo Manispaa ya Moshi wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua
utekelezaji wa shughuli za MKURABITA mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wafanyabiashara wa
Manispaa ya Moshi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza
nao kabla ya Waziri huyo kuzindua rasmi kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara
Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua
utekelezaji wa shughuli za MKURABITA mkoani Kilimanjaro.
Mratibu wa Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), CPA. Dkt.
Seraphia Mgembe akielezea majukumu ya taasisi yake kabla ya Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista
Mhagama kuzindua kituo Jumuishi
cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kilichopo Manispaa ya Moshi mkoani
Kilimanjaro wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri Jenista ya kukagua
utekelezaji wa shughuli za MKURABITA mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wa Manispaa ya Moshi mara
baada ya kumaliza kikao na wafanyabiashara hao kabla ya kuzindua kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara
kilichopo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya
kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za MKURABITA mkoani Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment