Tarehe 18 Oktoba, 2022
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) Mhe. Abdallah Chaurembo kupitia kamati yake ameipongeza Idara ya Kumbukumbu na
Nyaraka za Taifa kwa usimamizi mzuri na uadilifu katika matumizi ya fedha za miradi
ya maendeleo walizotengewa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2021, ambapo
idara hiyo imeokoa kiasi cha shilingi milioni 800 ambazo zimeelekezwa katika
maeneo mengine kuwahudumia wananchi.
Akiongoza kikao kazi cha kamati yake
kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu
na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka
2021/2022, Mhe. Chaurembo amesema ni wazi kuwa, usimamizi mzuri, uadilifu na
uaminifu wa watendaji wa Idara ya KumbuKumbu na Nyaraka za Taifa ndio
umewezesha kuokoa shilingi milioni 800 kati ya bilioni mbili walizotengewa na Serikali.
“Katika uongozi wangu nikiwa ni
Mwenyekiti wa kamati hii ya USEMI, sijawahi kuona taasisi iliyoonesha uadilifu
wa namna hii kwenye matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo, miradi yote
iliyopangwa imetekelezwa na mmeokoa milioni 800 ambazo ni fedha nyingi,” Mhe.
Chaurembo amesisitiza.
Mhe. Chaurembo ameipongeza pia Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuisimamia vema
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa iliyoweza kuwa mfano bora katika
matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya
USEMI ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Mhe. Pro. Palamagamba Kabudi amesema Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za
Taifa ni taasisi muhimu itakayoliwezesha taifa kutunza historia, urithi,
tamaduni, mila na desturi zake.
Aidha, Mhe. Prof. Kabudi ameishauri
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kutafuta na kutunza nyaraka za viongozi
ambao waliwasaidia waasisi wa taifa kuijenga nchi ili vizazi vijavyo viweze
kutambua na kuthamini mchango wao.
Naye, Mkurugenzi wa Idara ya
Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi amesema kama Sheria ya
Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Na. 3 ya Mwaka 2002 inavyoelekeza, idara yake inaendelea
kutafuta nyaraka zote muhimu zenye historia ya taifa ili kuzikusanya na kuzitunza
kwa manufaa na rejea ya taifa.
Bw. Msiangi ameongeza kuwa, idara
yake imekusanya nyaraka nyingi za viongozi waliowasaidia waasisi wa taifa
katika kutekeleza majukumu yao na bado inaendelea na mchakato wa kuzikusanya
ili historia ya taifa isipotee.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala
na Serikali za Mitaa (USEMI) imepokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa pamoja na Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kamati hiyo
katika kusimamia utendaji kazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akiongoza kikao
kazi cha kamati yake leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya
utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Utawala na Serikali za Mitaa na baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa leo jijini Dodoma kilicholenga
kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za
Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha
2021/2022.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ACP
Ibrahimu Mahumi akitambulisha watendaji alioambatana nao kwenye kikao kazi
cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa leo jijini Dodoma
kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu
na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa
fedha 2021/2022.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akichangia hoja
wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa
ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mhe. Mwantumu
Zodo akichangia hoja wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga
kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za
Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha
2021/2022.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Makete, Mhe.
Festo Sanga akichangia hoja wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dodoma
kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu
na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa
fedha 2021/2022.
Kamisha wa Maadili, Mhe.
Jaji Sivangilwa Mwangesi, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi
yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea
taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa
na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Mkurugenzi wa Idara ya
Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi cha
kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa
majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
No comments:
Post a Comment