Tarehe 19 Oktoba, 2022
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) Mhe. Abdallah Chaurembo amesema Ofisi ya Rais-UTUMISHI ikisimamia kikamilifu
utekelezaji wa Kanuni ya 61(4)
ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2022 itawezesha kutatua changamoto ya
watumishi wa umma kuonewa, kwani kanuni hiyo imetungwa kuiwezesha Tume ya
Utumishi wa Umma kutoa uamuzi wa mashauri ya kinidhamu kwa kutumia vielelezo
vya upande mmoja ikiwa upande mwingine utachelewesha vielelezo bila sababu za
msingi.
Mhe. Chaurembo ametoa maelekezo hayo
leo jijijni Dodoma, wakati akiongoza kikao kazi cha kamati yake kilicholenga
kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma na
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa mwaka 2021/2022.
Mhe. Chaurembo amesema, ni wajibu wa
Ofisi ya Rais-UTUMISHI kuhakikisha Kanuni hiyo iliyopitishwa na Bunge inatekelezwa kama
ilivyokusudiwa ili iwe na tija, ikizingatiwa kwamba wapo baadhi ya waajiri, viongozi
na watu wenye mamlaka wanaokiuka kwa makusudi taratibu za kuwaachisha kazi
watumishi wa umma na kuamua kutowasilisha vielelezo vya mashauri ya kinidhamu
Tume ya Utumishi wa Umma ili vitumike kutolea maamuzi.
“Ni wazi kuwa kanuni hii ya 61(4) ya
Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2022 inaenda kutatua tatizo la watumishi wa
umma kuonewa na kwa kufanya hivyo, mtakuwa mmeunga mkono kwa vitendo dhamira
njema ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha watumishi wote
wanatendewa haki na hatimaye kufanya kazi kwa amani na morali ya hali ya juu
katika kuwahudumia wananchi,” Mhe. Chaurembo amesisitiza.
Akizungumzia changamoto zinazowakabili
watumishi wa umma, Mjumbe wa Kamati ya USEMI ambaye pia ni Mbunge wa Urambo,
Mhe. Margaret Sitta amehoji uwepo wa idara au kitengo maalum katika Ofisi ya
Rais-UTUMISHI ambacho kimepewa jukumu la kushughulikia malalamiko ya watumishi
wa umma kwa wakati kama ambavyo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa
akielekeza mara kwa mara.
Akijibu hoja iliyowasilishwa na Mhe.
Sitta, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema ofisi yake ina idara ambazo zinasimamia
ushughulikiaji wa malalamiko katika utumishi wa umma ambazo ni Idara ya
Usimamizi wa Maadili, Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma na Kitengo cha
Sheria pamoja na Tume ya Utumishi wa Umma ambayo inashughulikia rufaa na
malalamiko ya watumishi wa umma.
Aidha Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa ofisi
imeanzisha Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call Centre) kwa ajili ya kuwawezesha
watumishi wa umma na wananchi kuwasilisha malalamiko yao pamoja na Mfumo wa
SEMA NA WAZIRI WA UTUMISHI ambao unatoa fursa kwa watumishi wa umma na wananchi
kuwasilisha malalamiko yao ili yaweze kufanyiwa kazi.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) imepokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kamati hiyo katika kusimamia utendaji kazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akiongoza kikao
kazi cha kamati yake leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya
utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma na Sekretarieti ya Ajira
Katika Utumishi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akijibu
hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa
ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma na Sekretarieti ya Ajira
Katika Utumishi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Katibu wa Tume ya
Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa
majukumu ya taasisi yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo leo jijini
Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya
Utumishi wa Umma na Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa mwaka wa
fedha 2021/2022.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma,
Bw. Hassan Kitenge akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi
yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea
taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma na Sekretarieti
ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Denis Londo akichangia hoja
wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea
taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma na Sekretarieti
ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akifafanua
hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa
ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma na Sekretarieti ya Ajira
Katika Utumishi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akiteta na
Makamu Mwenyekiti wa Kamati yake, Mhe. Denis Londo wakati wa kikao kazi cha
kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa
majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma na Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi
wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha
Mafuwe akichangia hoja wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga
kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma na
Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini,
Mhe. Michael Mwakamo akichangia hoja wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini
Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi
wa Umma na Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa mwaka wa fedha
2021/2022.
No comments:
Post a Comment