Na. Veronica Mwafisi-Arusha
Tarehe 10 Oktoba, 2022
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amewataka Viongozi na Watendaji katika taasisi za umma kusimamia kikamilifu rasilimaliwatu ili kuepusha migogoro sehemu za kazi kwa ustawi wa taifa.
Mhe. Jenista amesema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Arusha, Jiji na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua kero na changamoto zinazowakabili watumishi wa umma mkoani humo.
Mhe. Jenista amesema migogoro katika sehemu za kazi mara nyingi inatokana na watumishi wa umma kutotendewa haki katika kupatiwa stahiki zao, hivyo ni wajibu wa viongozi na watendaji kusimamia rasilimaliwatu hii kikamilifu ili kuepusha migogoro hiyo ambayo sio ya lazima katika sehemu hizo za kazi.
“Viongozi na watendaji waliopewa madaraka ya kuhakikisha eneo la kazi linakuwa salama, lenye amani, utulivu na lenye kuleta tija kwa taifa wakitimiza majukumu yao ipasavyo, migogoro mingi sehemu za kazi haitakuwepo na kila mtumishi atafurahia kufanya kazi katika eneo lake.
Mhe. Jenista ameongeza kuwa hakuna sababu ya kuwafanya watumishi wakate tamaa na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa kuwanyima haki zao za msingi.
Amesema ni wakati sasa wa viongozi na watendaji wa taasisi za serikali kuiga kwa vitendo yale yote yanayofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wa ngazi za juu katika kuliletea taifa maendeleo.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anaongoza kwa vitendo, hivyo ni wakati sasa wa kubadilika, tuuvae uzalendo anaoudhihirisha Rais wetu kwa vitendo, kila mmoja ajisikie anadaiwa kutekeleza wajibu wake na anayeishi kwa kuwanyanyasa anaowaongoza aache mara moja kwani ni dhambi kubwa,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mhe. Jenista ameongeza kuwa, watumishi wa umma wanapatikana kwa kuzingatia uwezo walionao na kwa kuwapanga kwa lengo la kujenga uchumi wa taifa na kuleta maendeleo endelevu, hivyo hawatakiwi kukutana na vikwazo vinavyowakatisha tamaa bali wakutane na mazingira wezeshi yanayowapa ari na kusonga mbele katika kutekeleza majukumu yao.
Mhe. Jenista ameongeza kuwa, mchango mzuri unaotolewa na watumishi wa umma katika kuliletea taifa maendeleo unatambulika na viongozi wa ngazi za juu akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na ndio sababu ametoa kipaumbele kwa watumishi wa umma kupatiwa stahiki zao kwa wakati.
“Dira na maono ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni kuwa na utumishi wa umma wenye kuleta tija kwa taifa na ndio maana amekuwa akijali masilahi ya watumishi ili kufikia malengo yake akiamini bila rasilimaliwatu yenye ubora basi rasilimali nyingine haziwezi kutekelezeka, hivyo ni wajibu wa viongozi na watendaji kusimamia masilahi ya watumishi kama ambavyo Mhe Rais ameleekeza.” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mhe. Jenista ameanza ziara ya kikazi
ya siku tano ya mkoani Arusha yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji na kutatua
kero na changamoto zinazowakabili watumishi wa umma pamoja na kukagua
utekelezaji wa miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za
Wanyonge (MKURABITA).
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akizungumza na Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Arusha,
Jiji na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Arusha
iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi
hao.
Watumishi
wa Sekretarieti ya Mkoa wa Arusha, Jiji na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara
ya kikazi ya Waziri huyo mkoani Arusha iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na
kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Said Mtanda, akitoa salamu za Mkoa wa Arusha kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama
mkoani Arusha iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi wa mkoa huo.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Missaile Musa, akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji ya mkoa wake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya
kikazi ya Waziri huyo mkoani Arusha iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua
changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akikaribishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Missaile
Musa, alipowasili mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya kikazi iliyolenga
kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa
huo.
Afisa
Biashara, Halmashauri ya Jiji la Arusha, Bw. Daudi Charles, akiwasilisha hoja
kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo mkoani Arusha
iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi
wa mkoa huo.
No comments:
Post a Comment