Friday, January 11, 2019

WATUMISHI WA TASAF WAELEKEZWA KUZIHUDUMIA VIZURI KAYA MASKINI ILI KUZIWEZESHA KAYA HIZO KUJIKIMU KIMAISHA NA KUONDOKANA NA UMASKINI



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Maendeleo  ya Jamii (TASAF)  (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga akieleza  majukumu ya taasisi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)  wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa TASAF kilichofanyika Makao Makuu ya TASAF jijini Dar es Salaam chenye lengo la kuhumiza uwajibikaji.

Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Maendeleo  ya Jamii (TASAF) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo  ya Jamii (TASAF) mara  baada ya kuzungumza na watumishi wa mfuko huo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. 

Wednesday, January 9, 2019

WATUMISHI WA TAKUKURU NCHINI WATAKIWA KUTOTUMIKA VIBAYA KUKWAMISHA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA NA UFISADI ILI KULINDA RASIRIMALI ZA NCHI


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi TAKUKURU (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kuhimiza mapambano dhidi ya rushwa.
Baadhi ya watumishi wa TAKUKURU makao makuu wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)  wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembelea  watumishi hao ofisini kwao jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kuhimiza mapambano dhidi ya rushwa.


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani kabla ya kuzungumza na watumishi wa TAKUKURU kwa lengo la kuhimiza mapambano dhidi ya rushwa  wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi hizo jijini Dar es Salaam  

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya TAKUKURU baada ya  kuzungumza na watumishi wa TAKUKURU kwa lengo la kuhimiza mapambano dhidi ya rushwa  wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi hizo jijini Dar es Salaam  

Tuesday, January 8, 2019

PTF YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA KWA KUWAPATIA MIKOPO KUNDI MAALUMU LA WALEMAVU, AKINA MAMA WAJASIRIAMALI NA VIJANA



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) wakati wa ziara ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji, ambapo pia alipata fursa ya kujionea wanufaika wa mikopo inayotolewa na mfuko huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikabidhiwa nyaraka mbalimbali na Mkurugenzi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Bi. Haigath Kitala mara baada ya mkurugenzi huyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji  wakati wa ziara ya kikazi ya Dkt. Mwanjelwa katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ziara ilikuwa na lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia bidhaa zinazotengenezwa na  kikundi cha Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi  Tanzania (FUWAVITA), kikundi cha UWAZI  SHALOOM cha akina mama wasindikaji, Kikundi cha MAKINI FOOD SUPPLIES cha akina mama wasindikaji na kikundi cha MAB cha vijana  wakati wa ziara yake ya  kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza maelezo ya Bi. Rose Kalulika kuhusu bidhaa zinazozalishwa  na kikundi cha akina mama cha UWAZI SHALOOM  wakati wa ziara ya  kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwasisitiza watumishi wa PTF kutoa huduma nzuri  kwa walengwa wa mikopo inayotolewa  na PTF wakati wa ziara ya  kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.