Na. Antonia Mbwambo na Veronica Mwafisi-Dar es salaam
Tarehe 22 Januari, 2026
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete amewatembelea na kuwajulia hali Mama Salma Omar Ali Juma, Mjane wa Hayati Dkt. Omar Ali
Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyumbani kwake
Msasani jijini Dar es Salaam na Mama
Regina Lowassa, Mjane
wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam
leo Januari 22, 2026.
Mhe. Kikwete amesema, Ofisi ya Rais-UTUMISHI inazingatia maelekezo ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya
kuthamini mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu pamoja na wajane wa
Viongozi hao Wastaafu ikiwa ni pamoja na kuwatunza kwa mujibu wa Sheria.
Kwa upande wake, Mama Regina Lowassa, Mjane wa Hayati
Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemshukuru na
kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia ya
Hayati Edward Lowassa wakati wote bila kuchoka.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akizungumza jambo na Mama Salma Omar Ali Juma (kushoto), Mjane wa Hayati Dkt. Omar Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akifurahia jambo na Mama Regina Lowassa (kulia), Mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati alipomtembelea nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 22 Januari, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akifurahia jambo na
Mama Salma
Omar Ali Juma (wa pili kutoka kulia), Mjane
wa Hayati Dkt. Omar Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Wengine ni Wakurugenzi na
Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mama Regina Lowassa, Mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake
Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Dawati la Viongozi wa Kitaifa
Wastaafu, Bi. Nyasinde Mukono (kushoto) akifurahia jambo wakati Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipomtembelea Mama Salma Omar Ali Juma (hayupo pichani), Mjane wa Hayati Dkt. Omar
Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwake Msasani
jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu
yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
Mama Regina Lowassa (katikati), Mjane
wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania wakati Waziri huyo
alipomtembelea nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari,
2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mama Salma Omar Ali Juma (kushoto), Mjane wa Hayati Dkt. Omar Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Dawati la Viongozi wa Kitaifa
Wastaafu, Bi. Nyasinde Mukono
(hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipomtembelea Mama Regina Lowassa, Mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania nyumbani kwake Masaki Jijini Dar
es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 22
Januari, 2026.
Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza na Mama Regina Lowassa Mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania wakati Waziri huyo
alipomtembelea nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari,
2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na Mama
Salma Omar Ali Juma (wa pili kushoto), Mjane wa Hayati Dkt. Omar
Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2026. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bi. Hilda Kabissa na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Dawati la Viongozi wa Kitaifa
Wastaafu, Bi. Nyasinde Mukono.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiagana na Mama Regina Lowassa, Mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati alipomtembelea nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 22 Januari, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiagana na Mama Salma Omar Ali Juma, Mjane
wa Hayati Dkt. Omar Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wakati alipomtembelea nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni
utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 22 Januari, 2026








No comments:
Post a Comment